Site icon A24TV News

Wananchi siha watakiwa kufanya mazoezi ili kuondoa changamoto dhidi ya magonjwa yasiyo ambukizi.

Na Bahati Siha,

Mratibu wa magonjwa yasiyo ambukiza Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Jonas Kira,ametoa rai kwa Wananchi Wilaya humo,kufanya mazoezi mara kwa mara ili kufanya miili yao kuwa imara na kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyo ambukiza

Haya ameyasema leo katika uwanja wa CCM Sanya juu Wilayani humo,wakati wa kufanya mazoezi mbalibali ikiwamo zoezi la kukimbia kwa Watumishi wa halmshauri,Jeshi la police,jeshi la akiba pamoja na Wananchi liliandaliwa na ofisi ya mkurungenzi mtendaji wa halmshauri hiyo.

Akizungumza mara baada ya kupata frusa,amewataka Wananchi Wilayani humo kujiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuifanya miili yao kuwa imara na kujikinga dhidi magonjwa yasiyo ambukiza

Amesema kumekuwa na ongezeko la kasi ya magonjwa yasiyo ambukiza,ikiwamo kisukari na shinikizo la damu,(PRESHA), kwa Wananchi na matibabu yake yakigharimu fedha nyingine sana kitu ambacho ni hatari

Kira amesema ukifika katika hospital zetu kwa sasa baadhi ya magonjwa yanayoongoza ni magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu , asilimia 9 ya wagonjwa wanaohudhiria katika idara ya magonjwa ya nje ni magonjwa yasiyo ambukiza

Amesema asilimia 33 ya wagonjwa wanaofariki idara ya magonjwa ya ndani yanasababishwa na magonjwa yasiyo ambukizwa , kwa hiyo ili ni tatizo,lazima tuchukue hatua,kauli mbio ya wiki hii inasema muda sasa tuzuie magonjwa yasiyo ambukiza

“Ni kweli leo tumefanya sehemu moja ya kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza,kwa maana ya mazoezi,ili kupambana na magonjwa hayo,tunatakiwa mazoezi yawe kwenye utaratibu wa maisha yetu”amesema Kira

Hivyo kuwaomba Wananchi kubadilika ,kuangalie mtindo wa maisha,lakini tuangalie ulaji unaofaa vyakula utoka makundi sita,nafaka,mizizi,ndizi mbichi, vyakula vya asili ,mbago mboga,matunda. na mengine kwa kufuata utaratibu wa wataalumu unavyotaka tutaweza kusalimika na magonjwa hayo.

Mkurungenzi mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi, ametoa pongezi kwa Wananchi na watumishi kujitokeza kwa katika mazoezi ya leo kwa ajili ya kujenga miili yao na kwamba mazoezi hayo ni endelevu na kuwataka Wananchi kujitokeza katika uchunguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu

Kwa hiyo November 27 mwaka huu kwa pamoja tunaweza kutekeleza jambo hili muhimu ambalo litapelekea kuchagua Viongozi wetu ambao watatusaidia kuongeza kipindi kingine katika kupanga mipango mbalibali ya maendeleao,tuhamasishane siku hiyo,

Kwa upande wake Zakia Shuma mkuu wa Jeshi la police Wilayani humo, amesema tunaelekea katika uchanguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu,kila mtu ni mdau kwenye hili jambo,tunaomba tutoe ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha usalama katika zoezi la uchaguzi.

Amesema kama unapata taarifa zozote ambazo zinaviashiria ya uvujifu wa amani,sisi tupo toa taarifa

Tunaamini sote hapa Siha ni yetu iwe salama kipindi cha uchanguzi,kwa hiyo tushirikiane kwa hali na mali ,tutakuwa na Askari kata ,jeshi la akiba kila kituo kwa ajili ya kuimarisha usalama,kila mtu anahaki ya kupiga kura akiwa salama,sisi tupo Kwa ajili ya kuhakikisha usalama

Mwisho