Site icon A24TV News

Wanawake jamii za asili wakutana Arusha kujadili changamoto zao.

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Wanawake Jamii za Asili Nchini wanakutana jiji Arusha kujadili changamoto zao ikiwepo athari za mabadiliko ya Tabianchi.

Wanawake hao kutoka jamii za wahadzabe, Wamasai, wabarbaigi,wadatoga na waakei wanasema mabadiliko ya tabia nchi yameleta ukame katika maeneo mengi ya jamii hizo na hivyo kuathiri maisha yao.

Akifungua Kongamano la siku mbili la wanawake wa jamii za Asili, Mkurugenzi wa shirika la utafiti na maendeleo ya jamii (CORDS) Lilian Looloitai amesema kuwa wanawake wa jamii za Asili wanakabiliwa na athari za mabadiliko ya Tabianchi yaliyopelekea kuwepo na vikwazo vya kiuchumi na kijamii.

Amesema mabadiliko ya Tabianchi yameathiri maisha ya kila Siku kwa wanawake wafugaji na waokota matunda na hivyo ni muhimu kwa wanawake hao kuwa na mtandao wa pamoja utakaosaidia kufikia malengo ya uongozi na maendeleo ya uchumi kwa jamii hizo.

Mtandao huo utatoa fursa kwa wanawake wa Asili kuwa na ujasiri wa kugombea nafasi za uongozi pamoja na kut Mawasiliano ya jamii zote . Mjumbe wa Bodi ya CORDs Adam ole Mwarabu akizungumza katika kongamano hilo alitaka wanawake wa jamii ya asili kuendelea kutunza mila na tamaduni zao.
Ole Mwarambu amesema licha ya maendeleo makubwa ya Sayansi ma teknolojia bado kuna haja ya kuendelezwa mila na desturi za jamii za asili. Amesema jamii za asili zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwepo masuala ya mabadiliko ya tabia nchi lakini umoja na mshikamano itasaidia kutatua changamoto hizo.
Regina Majawa Gapchojiga kutoka jamii za wa barbaigi anasema kuwa wanawake wa jamii hiyo Wameathiriwa mno na mabadiliko ya Tabianchi yaliyosababisha mifugo kufa na hivyo kulazimika kuhamisha iliyopo kwenda kutafuta malisho nje ya wailaya ya Hanang’ na hivyo kuathiri uchumi wa kaya zao.

Naye Janeth Kamunyu Toka shirika la Kinyok Indigenous Pastoralists women Organization (KIPWO) lililopo Mvomero Mkoani Morogoro anasema Kongamano hilo litawasaidia kuwa na sauti ya pamoja kujua changamoto zinazowakabili wanawake wa Asili Nchini Tanzania.

Afisa Masuala ya jinsia wa shirika la CORDS Martha Katau amesema kongamano hilo ni muhimu kwani limekutanisha wanawake wa jamii za asili nchini. Katau amesema wanajadiliana utatuzi wa changamoto za jamii za asili nchini.

Anna Matinda Afisa Utawala CORDS amesema wanaimani kongamano hilo litasaidia kuwaunganisha wanawake na kuwa na sauti moja katika utetezi wa jamii za asili. Alisema CORDS imeandaa kongamano hilo la kwanza pia kuwatambua wanawake wa jamii za asili shughuli zao mbalimbali na jinsi ya kuwaunganisha.
Nan’gida Laizer amesema changamato za jamii za asili ni nyingi hivyo CORDS kuwakutanisha ni jambo jema sana. Nan’gida alisema miongoni mwa changamoto ambazo wanakabiliana nazo ni athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Kongamano hilo la kwanza kwa wanawake wa jamii za asili linatarajiwa kufanikisha kuanzishwa kwa mtandao wa wanawake.wa jamii za asili nchini.

MWISHO