Site icon A24TV News

Baraza kuu la Waislmu Tanzania BAKWATA Wilayani Hai,lasema uchaguzi ulienda salama

Na Bahati Hai,

Waziza na walezi Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Wametakiwa kuwapa elimu ya Dini watoto wao ili elimu hiyo iwe Muongoze ya kutenda mema na kuzuia matendo maovu hapa Duniani

Haya yamesemwa na Immamu Muhamedi Hamza kutoka Wilayani ya siha mkoani hapa katika Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhamedi (SAW)yaliyofanyika katika Msikiti wa Kingereka B Bomang’ombe Wilayani humo,na kuhudhuria na Waumini ,Viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali.

Azingumza mara baada ya kupata frusa ,Immamu Muhamedi k hapa, ameomba jamii kuwekeza katika elimu ya Dini ili kupata waje wema na waadilufu katika Nchi hii na Dunia kwa ujumla

“Ni kweli kuwapa elimu , lengo la kuwepo kwa Dini ili kumuongoza mje katika kufanya matendo mema na kuzuia kufanye vitendo viovyo ,haya ndiyo malengo ya Dini ,”Amesema

Amesema elimu ndiyo bustani yenye kulea Taifa lilikuwa na Amani ,ambalo haliitaji kushikiwa rungu wala nini ,kwa mtiririko wanao kuzwa kwao wanakuwa watu salama ,maadili yatakuwa salama na Nchi itakuwa salama

Amesema watu wakifahamu malengo ya Dini Kwa ufasaha itasababisha kuwepo na Amani Duniani ,watu watapendana,watafanyiana mazuri na mambo mengine mengi,

Amesema kinyume na hapo ndiyo unaona yanajitokeza Duniani,maovu yametawala , ,tunapoteza kitu kikubwa sana kwa kuona Madrasa ni kitu cha kawaida jambo ambalo sio kitu kizuri,kwa hiyo malezi ya hizi bustani zina takiwa ziangaliwe kwa undani elimu ya Dini ipewe kipaumbele

Kwa upande wake ,Mwenyekiti wa BAKWATA Wilayani humo Omar Mahmudu,ameomba wazazi kusimamia watoto kwenda Madrasa,amesema watoto wanakwenda Madrasa siku wanayotala wao sio vizuri , Wazazi hatupo tayari kusimamia Dini

Viongozi wa Msikiti yote simamieni hili ,hakikisheni watoto wanaenda Madrasa na kupata masomo,siku ya kiyama mtakwenda kuulizwa kuhusu hili ,hivyo naomba tupeleke watoto Madrasa wapate kuelewa Dini yao.

Aidha ameipongeza uchunguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika November 27 mwaka,kwamba haukuwa na Dosari katika Wilaya hiyo

Amesema kuna watu wanataka kuposha potosha kwa sababu,hata siku moja mkienda wawili au watatu mnashindania kitu,anayeshindwa hakubali kuwa kumekuwa na haki,lazima atazusha mambo, tuache kuzusha tukubali matokeo.

 

Serikali imesimamia vizuri nafikiri ushahidi mzuri ni hapa Mtaa wa Kingereka B chama cha upinzani kimeshinda,hivyo kwa ujumla uchanguzi umeenda vizuri ,kilichobaki ni kumuomba Mungu uchanguzi utakafanyoka mwakani nao uende vizuri wa kuchagua Wabunge, Madiwani na Rais

Mwisho