Site icon A24TV News

JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMLAWITI RAFIKI YAKE BAADA YA KUMLEWESHA POMBE

Siha,

Mahakama ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imemuhukumu Wilson Mollel (29),mkazi wa Majengo Sanya juu Wilayani humo,mkulima kwenda jela kutumikia miaka 30 kwa kosa la kumuingilia kinyume na maumbile mwanaume wa miaka (45)ambaye walikuwa wakiishi wote chumba kimoja

Hukumu hiyo imetolewa December 12 mwaka huu na Hakimu mkazi mwandamizi wa mahakamani hiyo ,Elibahati Petro.

Mwendesha mashitaka wa serikali Kurwa Mungo , amesema tukio hilo lilitokea Junuary 2024,katika eneo hilo la Majengo majira ya jioni ,na kwamba kesi hiyo ilikuwa na mashahidi 6 akiwamo muhanga mwenyewe ,Daktari pamoja na Mwenyekiti wa eneo hilo

Kurwa amesema siku ya tukio mshitakiwa waliondoka na rafiki yake na kwenda kupata kinywaji pombe baa ,ambapo walikunywa na kulewa mshitakiwa baada ya kuona rafiki yake amelewa alimchukua na kurudi naye wanapoishi

Baada ya hapo mshitakiwa alifunga mlango na kuanza kulawiti,baada ya kufanya kitendo hicho na pombe ilipoisha kichwani na kukuta amefanyiwa kitendo hicho alitoa taarifa kwenye vyombo vya Sheria

“Ni kweli mshitakiwa alipoona rafiki yake amelewa ndipo alichukua jukumu la kurudi hapo wanapoishi na kufunga mlango na kumuingilia kinyume na maumbili , jambo ambalo halikubaliki mbele ya mbele za Mungu ni kitendo kiovu”amesema Kurwa

Kurwa amesema kitendo hicho ni kinyume kifungo 154(1)(a)cha kanuni ya adhabu 16 iliyofanyiwa marejeo 2022,na kwamba kesi hiyo ya namba 1414/2024

Licha ya kuwa wakulima pia walikuwa wananishughulisha na uuzaji wa vyuma chakavu katika eneo hilo la Majengo SanyaJuu

Wakati wa kutoa hukumu hiyo Hakimu amesema ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo, unakwenda kutumikia kifungu cha miaka 30 jela

Mwisho