Site icon A24TV News

MAKAMU WA RAIS DKT PHILIP MPANGO AWATAKA TAKUKURU KUONGEZA NGUVU YA KUPAMBANA NA RUSHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

Na Geofrey Stephen .ARUSHA

MAKAMU wa Rais Dkt Philip Mpango amebainisha maeneo sita vinara yanayoongoza kwa rushwa nchini kuwa ni pamoja na sekta ya Ardhi, Polisi,ukusanyaji wa mapato serikali kuu na Halmashauri,utoaji wa Tenda,upat
ikanaji wa Leseni na upande wa chaguzi.

Dkt Mpango amebainisha hayo jijini Arusha wakati akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Takukuru nchini ,na kuitaka Taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini Takukuru, kuongeza nguvu katika maeneo hayo ili kutokomeza vitendo vya rushwa Nchini .

Alisema bado malalamiko kwa wananchi kunyimwa haki na kuombwa rushwa ni makubwa ,hivyo alitaka jitihada zaidi kwa Takukuru zifanyike.

Alisema taarifa za kila mwaka za Takukuru na PPRA zinathibitisha hayo.

“Kwa mfano katika taarifa ya ukaguzi ya mamlaka ya usimamizi wa umma PPRA kwa Taasisi 44 za umma zilizokaguliwa mwaka 2022/23 zinaonesha zabuni 15 zenye thamani ya sh, bilioni 67.27 zilitolewa kwa kutumia maelezo ya zabuni yenye kubagua baadhi ya wazabuni,lakini wazabuni walichagukuwa na kupewa mikataba 25 yenye thamani ya sh, bilioni 56.7 pasipo kuithinishwa na bodi ya zabuni”

Aidha alisema majadiliano ya mikataba 23 ya taasisi saba yenye thamani ya sh, bilioni 64.5 yalifanyika bila kuwepo kwa mpango wa mahojiano, lakini pia mikataba 60 yenye thamani sh, bilioni 54 ilisainiwa bila kuidhinishwa na ofisi mwanasheria mkuu wa serikali na mikataba 10 ya manunuzi kwenye Taasisi 5 yenye thamani ya sh, bilioni 7.48 iliongezewa muda bila kufuata utaratibu.,hivyo yote hayo yanadhihilisha kwamba taratibu za manunuzi hazikufuatwa na kuna vitendo vya rushwa.

“Hivyo naagiza Takukuru kufanyiakazi taarifa hizo na kuchukua hatua stahiki na viongozi wawe mstali wa mbele kuepuka vitendo vya rushwa vinavosababisha kurudisha nyuma jitihada za serikali ”

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Crispin Chalamila alisema ndani ya miezi 12 iliyopita Takukuru imeokoa fedha zaidi ya sh ,bilioni 18 kupitia operesheni mbalimbali za uchunguzi pamoja na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo huku akisema kuwa fedha hizo zilirejeshwa serikalini na nyingine kutumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kadiri ilivyokusudiwa na hivyo kuchangia katika ustawi wa wananchi.

 

Pia program ya Takukuru Rafiki imelenga kutambua na kutafuta majawabu ya kero katika utoaji wa huduma, kero ambazo zikiachwa bila kutatuliwa zinaweza kusababisha vitendo vya rushwa kwani programu hiyo imekuwa yenye mafanikio makubwa kadiri ya mrejesho wa wananchi wanaopokea huduma na wadau wanaotoa huduma.

Alisema Taasisi hiyo imeendelea kuchunguza tuhuma za vitendo vya rushwa na pale penye ushahidi na kwa kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) walifungua na kuendesha kesi mahakamani kwani Jamhuri imeshinda kesi kwa asilimia 75.9 tofauti na mwaka jana ambapo jamhuri ilishinda kesi kwa asilimia 67.7 katika kesi zilizotolewa maamuzi.

“Tunajua bado tuna safari ndefu kufikia wastani wa juu zaidi na hili ni jukumu mojawapo la mkutano huu kupata majawabu”

Pia watafanya shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kujitolea kuchangia damu ili kuwasaidia watu wenye uhitaji na vilevile watawatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru wakiwemo ‘watoto njiti’ pamoja na wale ambao wamekaa hospitali kwa muda mrefu na upandaji miti katika eneo la hospitali hiyo ili kuiunga mkono Serikali ya katika jitihada za kuhakikisha utunzaji wa mazingira unaendelezwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu alisema kipindi cha kuanzia mwaka 2022/2023 na 2024/2025 Takukuru iliajiri watumishi wapya 1,190 ikiwemo
magari mapya 195 yenye thamani ya sh, bilioni 39.174 ambayo yamesambazwa katika ofisi za TAKUKURU nchi nzima kulingana na mahitaji.

 

Pia majengo ya ofisi 23 yenye thamani ya jumla ya sh, bilioni 12.5 yamejengwa katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini,ikiwemo mikoa mitano ya Kilimanjaro, Simiyu, Iringa, Shinyanga, Morogoro naWilaya 18 Mvomero, Kongwa, Kilolo, Kiteto, Liwale. Momba Nyasa, Monduli, Kishapu, Rombo, Nzega, Nkasi, Kaliua, Rungwe, Mbulu, Ukerewe, Makete, Nyanghwale.

Aliongeza pia katika kuimarisha matumizi ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Takukuru imetandaza mifumo na kununua vifaa vya TEHAMA kwa jumla ya bilioni 3. 443,pia katika kuboresha mazingira bora ya mahali pa kazi, wawezeshwa kupata samani za ofisi za gharama sh, bilioni 3.901.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alisisitiza mkoa huo upo salama na unamsingi ya imani unaofanywa na viongozi wa dini pia kutakuwa na maombi ya siku tatu ya kukomboa ardhi ili wananchi waweze kupata haki zao juu ya ardhi

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtandao wa wabunge wa kupambana na rushwa Afrika,tawi la Tanzania(APAAC),cap George Mkuchika alisema wananchi bado wanaimani na takukuru na kuitaka Taasisi hiyo kutobweteka na baadhi ya mafanikio bali waendelee kutoa elimu na ukaguzi wa taarifa wanazotoa viongozi kuhusu umiliki wa mali zao.

Ends…