Site icon A24TV News

Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhamedi (SAW) kimkoa yafanyika Bomang’ombe Wilayani Hai

Na Bahati Hai,

Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), mkoa wa Kilimanjaro,limesema Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhamedi (SAW), kimkoa yafanyika Bomang’ombe Wilayani Hai mkoani hapa

Maulidi hayo ambayo yataanza Desemba 28,2024 hadi 2029 ,itatanguliwa na matukio ya kijamii ikiwamo zoezi la upandaji miti, uchangiaji damu pamoja na maonyesho ya wanafunzi yakiambatana na Michezo mbalimbali

Taarifa imetolewa Desemba 23,mwaka huu na sheikh wa mkoa wa Kilimanjaro Mlewa Kimwaga wakati Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo amewataka Waumini wa Kiislamu kujitokeza kwa wingi na hata wasiokuwa Waislamu wanaopenda kheir pia wanakaribishwa.

 

“Ni kweli kama nilivyosema tutafanya hadhara ya Maulidi kama nilivyosema Desemba 28,2024,litaanza zoezi la upandaji miti kuunga mkono jitihada za Serikali dhidi ya utunzaji mazingira, sambamba na utoaji damu ,hii yote ni katika Maazimisho kuzaliwa Mtume Muhamedi (SAW)”amesema Mlewa

Mlewa amesema Desemba 29,2024 ,ndiyo siku rasmi ya Maulidi ambapo yataudhuriwa na Waislamu wa Wilaya zote mkoa huu na nje ya mkoa

Hivyo amewasisitiza Waislamu wajitokeze kwa wingi katika hadhara hiyo ili kujakufanikisha jambo hilo adhimu ,ambapo kama alivyosema yafanyika Bomang’ombe eneo la uzunguni Msikiti mdogo karibu na anapoishi sheikh wa mkoa huu ,nawaombeni sana sana2

 

Katika Maulidi watu upata frusa ya kuelezwa yote aliyoyafanya Mtume Muhamedi (SAW),na wao kwenda kuyafanyia kazi

Katibu wa BAKWATA mkoani hapa Awazi Lema, amesema kutakuwa na Wageni mbali wakiwamo wa Serikali

Mwisho