Na Mwandiahi wa A24tv.
Kamanda wa Polisi wilaya ya Arusha (OCD)amepiga marufuku bodaboda kusafirisha wanafunzi pamoja na kuwataka wamiliki wa shule kuacha kusafirisha wanafunzi na mwalimu wa jinsia moja na badala yake kuwepo na jinsia mbili katika kila gari linalobeba wanafunzi .
Akizungumza kwa niaba ya (OCD) wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Georgina Matagi ASP Chate ambaye ni mkuu wa Kituo cha Murieti katika hafla ya kuwapongeza wahitimu wa Darasa la Saba ambao wamefanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la Saba Shule ya awali na Msingi Socrates iliyopo Mkoani hapo,alisema jukumu la jeshi hilo ni kuendelea kutoa elimu pamoja na kuwaadabisha wanaokika sheria.
“Ni marufuku bodaboda kusafirisha wanafunzi wa shule na tutambue tu usafiri huu siyo salama hasa unapobeba watoto wengi kwa wakati mmoja,unakuta bodaboda zinazungukia kila nyumba kukusanya watoto na kuwapeleka shuleni jambo ambalo hata wazazi wanaofanya hivyo hawajui thamani ya watoto wao”alisrma na kuongeza.
Alitolea mfano wa kesi ya ubakaji iliyopelekwa katika kituo hicho na kulipofanyika uchunguzi ilibainika kuwa usafiri uliotumika ,katika gari hilo la wanafunzi halikuwa na mwalimu wa kike hivyo anko ndiye aliyebanwa kwa maswali na haikuishia hapo walitafutwa hata waliompokea mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho nyumbani ambapo ilibainika kuwa ni Anko hakukuwa na jinsia ya kike nyumbani hivyo ikawa vigumu kuufahamu ukweli kwa haraka.
Naye mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Murieti Ngolo Matugolo alitoa rai kwa wazazi na walezi kulinda watoto wao msimu huu wa likizo,Sikukuu za mwisho wa Mwaka na wasiruhusu wageni hasa watu wazima kulala na watoto wanapokuwa wametembelea nyumbani kwa ajili ya likizo .
” Nitoe wito kwa wazazi na walezi sote tunafahamu huu ni mwisho wa Mwaka ni dhahiri kuwatunatembelewa na ndugu jamaa na marafiki, niwaombe tu msimwamini mtu hata kuacha watoto walale nao chumba kimoja .
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Joyce Msofe pamoja na mmoja wapo wa wazazi wakizungumzia suala la ukatili katika jamii waliwataka wazazi na walezi kuacha kukumbatia watoto wao tu na kuwasahau wawengine jambo ambalo limekuwa changamoto kuweza kurekebisha maadili katika Jamii.
Hata hivyo akieleza ugumu na Mafanikio ya utekelezaji wa Mtaala mpya Mwalimu mkuu wa shule ya Socrates Wycliffe Rioba alieleza namna ambavyo walipata shida kutekeleza mtaala kutokana na mfumo waliozoea wanafunzi ambapo kwa sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza mtaala huo..
Shule ya awali Socrates huamini kufanya mahafali baada ya matokeo ya mitihani ya taifa ya darasa la Saba kwa lengo la kuwapongeza wahitimu na kuwapa nasaha za kuanza hatua mpya ya elimu ya Sekondari ambapo wahitimu 8 walitunukiwa vyeti vya elimu ya msingi huku zaidi ya Wanafunzi 70 wa awali wakitunukiwa vyeti vya kuingia darasa la kwanza.
Mwishooooo.