Site icon A24TV News

Wananchi Siha wacharuka wataka gari ya zimamoto

Na Bahati Siha,

Wakazi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,wameomba serikali kuwajibika kwa kuwapatia gari ya zimamoto ili kuweza kukabiliana na majanga ya moto yanatokea mara kwa mara

Haya yamejiri baada ya kuonekana Wilaya hiyo kutokuwa na gari ,na linapotokea janga la moto magari hayo yanalazimika kutoka Moshi mjini kitendo ambacho kinalazimu kufika kwa kuchelewa na kukuta Mali zimeteketea kwa moto

Wakizungumza waandishi wa habari kwa nyakati tofauti,Wamesema upo ulazima kwa Wilaya kuwa na gari kutoka na moto kuzuka mara kwa mara na gari ya hiyo ya zimamoto kutoka nje ya Wilaya,

“Ni Wilaya haina gari ya zimamoto,moto unazuka sehemu inabidi gari hilo litoke nje ya Wilaya na kufika eneo la tukio kwa kuchelewak kwa sababu linatoka mbali ,tunaomba tupatiwe gari”Wamesema Wananchi hao

Joseph Kimario mkazi wa SanyaJuu akizungumzia jambo hilo,ameomba Serikali kulitizama jambo Kwa umakini ili kunusuru Wananchi kupata hasara kwa vitu vyao kuteketea kwa moto na kusababisha wengine kufilisika kabisa.

Akitokea mfano ya moto uliotokea juzi kwenye maduka ya bidhaa mbali mbali eneo la Kanisa Katoliki SanyaJuu ambapo maduka takiribani 5 yaliugua Wangewahi wangeweza kuokoa vitu vingi

“Ni kweli bidhaa nyingi wangeokoa ,hapa wamefika saa 1 na dadika 8 na moto ulianza saa 12 na nusu asubuhi unaona kunampishano mkubwa”amesema Kimario

Baraka Mmari mkazi Koboko Wilayani humo,amesema June 5 mwaka huu ,nyumba ya jirani yake ilikuwa inaungua kwa moto Ila Kwa jitihada za Wananchi waliweza kunusuru vitu kidogo ,lakini kama zimamoto lingekuwapo nadhani tungenusuru vitu vingi

Mkazi wa Ngarenairobi west Kilimanjaro Wilayani humo, Festo Asenga ,amesema kwa muda mrefu wa kazi wa Maeneo hayo wamekuwa wakisisitiza kuwepo kwa gari hilo,

Amesema majanga ya moto yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kusababisha hasara kubwa kwa Wananchi kwa nyumba kuteketea yote bila kuokoa kitu chochote,hasa kwenye nyumba hizi zilizojengwa mabanzi

Kwa hiyo tunaomba Wilayani yetu angalau ingekuwa na gari hilo ingesaidia sana kuokoa Mali tumechoka Kila mara vitu kuungua inaturudisha nyuma kimaendeleo

Paul Marigwa kutoka ofisi ya zimamoto na uokoji Wilayani humo, amesema walipata taarifa kwamba kuna moto umezuka hapo SanyaJuu na maduka yanateketea ,Ila chanzo chaka hakijahulikana

kwamba gari ya zimamoto inalazimika kutoka mjini Moshi mjini na thamani ya vitu vilivyougua bado haujatambulika,kutoka na yenye maduka kutokuwa na utulivu, pia kuna mtu mmoja alijeruhiwa kwa kuungua moto na yupo hospital

Egina Nzao Diwani wa viti maalumu,ameshuku Wananchi na Jeshi la police,jeshi la zimomoto pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa ushirikianona kuhakikisha wanaudhibiti moto huo ili usiendele kuleta madhara sehemu nyingine

Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka,alithibisha kutoka moto huo,nakuwataka Wananchi kuchukua tahadhari zote wanapotumia umeme wahakikishe kuzima vifaa inapofika majira ya usiku

Mwisho

 

 

 

Error Icon
Address not found
Your message wasn’t delivered to jaychume@yahoo.com because the address couldn’t be found, or is unable to receive mail.
The response from the remote server was:
554 30 Sorry, your message to jaychume@yahoo.com cannot be delivered. This mailbox is disabled (554.30).

Mwisho.