Site icon A24TV News

Wananchi wa kata ya Masama magharibi watakiwa kusherekea sikukuu kwa kudumisha amani na upendo

Hai,Wakati wakristo wakitarajia kuungana na wengine Duniani kusherekea sikuu kuu za mwisho wa mwaka ikiwamo Krisimas na mwaka mpya Wametakiwa kudumisha amani na upendo pamoja na kusaidiwa watu wenye uitaji

Pia kuacha kutumia sikukuu hizo kwa kutenda matendo yanayomchukuza Mungu ikiwamo kutumia dawa za kulevya kulewa na kuanza kutoa matusi hivyo na pia kuendesha vyomba vya moto kwa spidi

Diwani wa kata ya Masama magharibi Mashoya Natai,aneyabainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari walipotembea kata hiyo, ambapo amewaomba Wananchi kuwa na amani na upendo Kwa watu wakati wa sheree hizo.

“Ni kweli nawaombeni Wananchi wa kata hii na sehemu nyingine tusherekee sikukuu kwa kudumisha amani na upendo na kwenda kuwasaidia watu wenye uitaji na sio kutumia kwenda kufanya maovu amesema Natai

Kuna baadhi ya watu kwenye sherehe kama hizi wanazingeuza ni siku ya kufanya ufusika kufanya mambo maovu yasiyompendeza Mungu hii sio sawa hata kidogo,ni siku ya furaha

Hivyo nimeshauri kusherekea kwa furaha ,amani na upendo na kumtegemea Mungu ili kufikia mipango mbali mbali na hasa mwaka mpya unaokuja wa 2025

Natai amesema mwaka huo mpya unaokuja wa 2025,uwe mwaka wa mafanikio makubwa Kwa kila mmoja wetu na Kwa jamii yote,tuliyopanga tuyatekekeze kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu

Katika hatua nyingine Frank Kimario, mkazi wa kijijii cha Mashua amempongeza Diwani hiyo kwa utekezaji wa miradi katika kata Kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi October 2024,

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara,ujenzi wa vyumba vya Madrasa ,ujenzi wa vyoo ujenzi wa vituo cha Afya,bweni la wasichana ,ambayo hiyo imetekelezwa katika vijiji vya Mashua,losaa,Kyuu,lukani pamoja na Nkwansira,

Awali Diwani huyo, amesema kwamba mwakani wanatarania kutekeleza miradi mbali mbali kwenye kata hiyo, ikiwa ni kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2020

Amesema miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa daraja ,Saaashi,kiwanda cha losaa,Skimu ya bwawa la poloti, ujenzi wa bwani shule ya Sekondari Kyuu, ujenzi wa bwani shule ya Sekondari , Lukani ujenzi wa zahanati Kijijii cha Kyuu na miradi mingine mingi

Mwisho