Site icon A24TV News

Wanao jifungua mjini na kutekeleza watoto vijiji,watikiwa kuchukuliwa hatua kali .

Hai,Diwani wa kata ya Masama Magharibi Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro,Mashoya Natai amewataka baadhi ya Wasichana Wilayani humo,kuacha tabia ya kuzaa watoto mjini na kuja kuwatelekeza kwa wazazi wao vijijini na wao kurudi mjini ,kwani jambo hilo linawafanya watoto hao kukua katika mazingira magumu na hatarishi

Haya yamesemwa na Diwani huyo ,wakati wa sherehe fupi kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kituo cha lukani Children Center,kituo ambacho Diwani huyo ndiyo kiongozi ambapo watoto hao walipewa chakula na mavazi kwa ajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliudhuriwa na Wadau mbali mbali wa elimu pamoja na Baadhi ya wana jamii ,ameomba Wasichana kujizuia kuzaa bila kufuata utaratibu kitu ambacho kinawafanya kuja kuwatelekeza watoto kwa wazazi wao vijijini,na watoto kukua katika malezi yasiyo mazuri

Natai amesema kwa sasa ukienda kwenye vituo hivyo vya watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu, wanaoishi katika mazingira magumu wengi wao ni wale Wazazi wamewatelekeza wao na kukimbia maeneo ya mijini

Wito wangu kwa hao wanaowatelekezea Wazazi watoto wao,kama kweli maisha uko mjini yamekuwa magumu ,wanapowaleta basi angalau wawasapoti Wazazi kwa chochote kitu

“Ni kweli kuwatumia kitu kidogo kuwasapoti watoto wao ni jambo la kiungwana kabisa ,lakini wanawaachia kabisa wazazi bila kutumia kitu chochote ili jambo sio sawa,japo watakuwa lakini vitu vingi wanavikosa katika maisha yao

Amesema Wazazi wengine ni wazee na wamekuwa bibi na babu,waliochoka ambao hawana chochote, sasa bado unamuongezea watoto ,

Kwa hiyo tufuate utaratibu wa kupata hawa watoto na kuwatumza sisi wenyewe ,kwani inakuwa rahisi kuwaepusha na madhila mbali mbali ikiwamo vitendo vya ukatili dhidi yao

Kwa upanda wake Thomas Kudalisamu mchungaji wa Doyasisi ya kasikazini Jimbo la Hai usharika wa Ng’uni ,akizungumza mara baada ya kupata frusa hiyo, amesema hipo haja ya kupambana na tabia hiyo ikiwamo kwa Serikali ,Kanisa na jamii kuungana kupiga tabia hiyo ili watoto wapatikane kwa utaratibu unaotakiwa

“Ni kweli Wapo baadhi ya kina dada ambao wanapata watoto,na watoto wale wakati mwingine wanawapata wakiwa mjini ,wanapojifungua wanawaleta kwa wazazi vijijini

Na jambo hili limekuwa kama mzigo ,kwa wazazi wale ,kwa sababu wazazi tayari walishaifanya hiyo kazi ya kuwalea hao wazazi,lakini sasa ni kama wanakuja kuanza moja kulea vile vichanga na wale ni babu na bibi nguvu zimepungua

Amesema Mtoto kama huyo katika kukua kwake hakuna wa kumuonya na kumuelekeza ,sababu hiyo sasa umeanza kutokea maadili kuwa mabaya na hata kwenda anavyotaka ,kwa sababu hana uthibiti ule unaotoka kwa wazazi ,mtu ambaye anaweza kumuonya na hata akaweza kumthibiti

Thomas amesema kwa sababu bibi na babu ya hali halisi ya uzee , huyo Binti au kijana akichanganyika uko mitaani basi unaanza kuona maadili ya kijamii yakishuka

Lakini tatizo ili linaendelea wakati mwingine anapomuacha yule mtoto kuwa anaendelea kukuwa ,anarudi mjini, bahati mbaya analeta tena mwingine,kwa hiyo kwa sababu hiyo unagundua kabisa jamii inaelekea pasipo,

Sasa nini kifanyike tuthibiti hizi hali ,kwa sababu kama tutaendelea hivyo maana yake kizazi kitafika mahali hakutakuwa na kizazi chenye maadili kabisa

Amesema watu wataishi wanavyotaka ,sababu ili kuzibiti ni lazima ifike mahali ,Kanisa,Sarikali na wazazi kuwa na ushirikiano wa kuhakikisha kwamba tunatia maadili kwa hao vijana ,lakini Serikali ichukue nafasi yake

kama Serikali haitaliona jambo hili wakashirikiana na Kanisa na Jamii,basi mbele ya safari hali itakuwa ngumu,na itakuwa ngumu sana ,kwa hiyo tuombe Kila sehemu ichukue nafasi yake ,Kanisa ichukuwe nafasi yake likishirikiana na Serikali na jamii

Awali katika taarifa yake Mwalimu Easter Liyamuya amesema kituo hicho wapo watoto 91 ambapo amesema ukiweka na wale ambao tayari wapo shule za msingi na Sekondari wanafika zaidi ya watoto 155

Hiki kituo kinaendeshwa na Wadau mbali mbali ikiwamo marafiki ,tunaomba Serikali pia wafike angalau waangalie hata halmshauri yetu ya Hai watuunge mkono waje waone kazi wanazofanya za kijamii na kutuunga mkono.

Pia amewashukuru marafiki ambao wamejitolea kwa kufanyajitihada kuhakikisha watoto hao wanapata mahitaji na kuwa ni sehemu ya jamii

Mwisho.

 

Mwisho