Site icon A24TV News

wasijulikana wang’oa bikoni zilizowekwa na Bonde la Pangani eneo la Isanja Siha

Siha,

Mwenyekiti wa Jumuhiya ya watumia maji mto Sanya , Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro ,Goodchance Moshi,amesema wale wote waliong’oa bikoni eneo la Tindiga la Isanja kata Nasai Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro hatua kali dhidi yao itachukuliwa ili iwe fundisho kwa wengine

Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelea chanzo hicho cha maji Tindiga hilo la Isanja ,ambapo alishuhudia uharibifu mkubwa ambapo bikoni 17 zikiwa zimeng’olewa wasijulikana.

Mwekiti huyo ambaye pia ni mjumbe wa wa Bodi bonde la Pangani,akizungumza mara baada ya kutembea eneo hilo,amesema lazima hatua za kisheria dhidi yao zitachukuliwa Kwa lengo la kuokoa chanza hicho cha maji kugeuka jangwa

“Ni lazima wachukuliwe hatua kwa wale wote waliong’oa bikoni ,na watuhumiwa wa kwanza ni wale kwa namna moja au nyingine walikuwa ni wanifaika wa Maeneo haya kabla ya kuweka alama hizo”amesema Moshi

Moshi,amesema hatua hiyo itachukuliwa kwa sababu kabla ya kuweka alama hizo ,waliwaita Wananchi wanao zunguka eneo hilo la Isanja na kukaa na vikao na kuwaelimisha nia ya kuweka alama hizo na kutuelewa ,lakini hivi karibuni tumepata taarifa za kushangaza kwa wasamaria wema kwamba zile alama zimeng’olewa.

Sasa tunashangaa kwamba Serikali inatenga maeneo kwa ajili ya vyanzo vya maji ili maji ili Wananchi waweze kunufaika na maji,lakini sasa watu wanakuja kung’oa tena

Hawa Wananchi tunawalindia hivi vyanzo ,hawaoni umuhimu wa hivi vyanzo kwamba ni manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo,tutaendelea kutoa elimu na tutaendele kuchukua hatua hatuwezi kukaa kimya

Allfafanua kwamba bikoni zaidi ya 25 ziliwekwa ,lakini 17 wamezing’oa na eneo loliathirika sana ni upande Kijijii cha Nrau ndiyo haswa zilikong’olewa zote 17,uku wakifahamu fika kwamba kitendo hicho sio cha kiungwana kuharibu vyanzo vya maji

Kwa upande wake,John Mmari ,mkazi wa Kijiji hicho ,amesema eneo hilo kiasili maji yalikuwa hayakauki ,lakini kadiri m0iaka inavyoenda wananchi walilivamia na kuanza kilimo maji yamepungua yamebaki kidogo na wakati mwingine panakuwa hakuna maji kabisa kutokana na uharibifu na mifugo kuingizwa eneo hilo

Hellen Kileo amesema eneo hilo kwa muda mrefu wamekuwa wakinufaika na kilimo mbali mbali ikiwamo cha mboga mboga ,kama mchicha,mnavu,pamoja na pili pili hoho.

Amesema kwamba Jumuhiya hiyo ilifika na kuwapa elimu ya utunzaji wa chanzo hicho ili maji yaendelee kupatikana na wao kuendelea na kilimo hicho na kuweka alama ,lakini watu wachache wamezing’oa ,tunaomba sheria ichukue mkondo wake,kwa sababu elimu walipewa ili iwe fundisho kwa watu waharibifu wa mazingira

Awali mwenyekiti huyo ,amesema wao kama Jumuhiya ndiyo wanasimamia vyanzo vya maji eneo hili la Mto sanya ni pamoja na Matindiga,,Chemi chem,Miti,Mabwawa ni sehemu ya usimamizi wao kama Jumuhiya kuhakikisha vinabaki salama

Mwisho