Site icon A24TV News

DC CHIKOKA AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI SEKTA YA UTALII

Na Richard Mrusha Musoma.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka Amesema wanakaribisha wawekaji kuwekeza kwenye fukwe zilizopo ndani ya ziwa Victoria wilaya ya Musoma mkoani Mara kwani kuna vivutio bora.

Hayo ameyasema Januari 3,2025 alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walitembelea ofisini kwake.

Amesema katika kurahisisha usafiri wanaendelea kukamilisha ujenzi wa uwanja wa ndege ambao utasaidia kukuza uchumi wa wilayani na mkoa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa utakapo kamilika uwanja huo utarahisisha watalii kufika katikati Hifadhi yaTaifa Serengeti kwani kutoka Musoma kwenda Hifadhini hapo kuna umbali wa kilomita 70 tu kulinganisha na mikoa mingine.

Chikoka amesema anamshukuru Mkurugenzi wa Legrand Victoria Hotel kwa uwekezaji alioufanya na wao kama serikali wataendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha

Na kwa upande wake Mkurugenzi wa legrand Victoria hotel Ramadhani Msomi
amatoa wito kwa Mhe Rais DKT Samia Suluhu Hassan kuwa ucheleweshwaji wa kuto kamilika ukarabati wa uwanja wa ndege mkoani Mara unachangia kurudisha nyuma idadi ya watalii kutokana na umbali marefu.

Amesema uwanja wa ndege ukikamilika utachochea idadi kubwa ya watalii kwani mkoani Mara kuna vivutio mbalimbali ikiwemo hifadhi ya Taifa Seregetia, fukwe,na Makumbusho ya Baba wa Taifa ambavyo vinavutia watalii kuja kutembelea.

Amesema watalii wamekuwa wakitumia gharama kubwa kuja mkoani hapa kutokana na kutokamilika kwa uwanja hali ambayo inakoseha mkoa mapato na Taifa kwa ujumla.

Amesema kutokana na mhe Rais kuzindua filamu ya The Royal Tour imesaidia Sekta kukuwa kwa kasi hali inayopelekea uwekezaji kukuwa zaidi.

Ameongeza kuwa kupitia uwekezaji huo ameweza kuzalisha ajira zaidi ya 50, na anaendelea na ujenzi wa hotel pamoja na Nyumba za kupangisha (Apatimenti)

Kwa upande wake meneja wa Legrand hotel Paul Mutinda amesema wamekuwa wakipokea wageni kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ambao wanapendelea kuona vivutio mbalimbali

Moja ya vivutio ambavyo watalii hupendelea kama vile uvuvi wa kutumia ndowano ndani ya ziwa Victoria ,kutazama ndege wa aina mbalimbali waliopo ziwani pamoja na kwenda shule aliyosoma Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere na makumbusho yake Wilayani Butiama.

Ameongeza kuwa mbali na kutembeza watalii hao katika vivutio mbalimbali pia wamekuwa wakipika vyakula vya asili ya Mkoa wa Mara kama vile ugali wa mtama ,nyama choma na kichuri pamoja na vyakula vya mataifa mbalimbali.

 

Mwisho.