Hai,
Mkuu mpya wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Hassani Bomboko,amewataka Watendaji wa Kata vijiji,Wakuu wa idara ,watumishi wa Taasisi za Serikali Wilayani humo , kutokukaa ofisini muda mwingi na badala yake watoke na kuwapelekea huduma Wananchi
Kauli hiyo ameitoa wakati makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Lazaro Twange ambaye kwa sasa amahamishiwa Wilayani ya Ubungo jijini Dar es salaam , yaliyofanyika katika ukumbi wa halmshauri hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisini , amewataka watumishi hao muda mchache kuwa ofisini na muda mwingi kuwekeza katika kutatua kero za Wananchi
Bomboko amesema Wananchi wengi maeneo mbali mbali ikiwamo vijijini wanachangamoto ,wanakero wanamaswala mbali mbali yanayohitajika utatuzi kutoka Serikalini,lakini ukikaa ofisini hatuwezi kufahamu hayo,
“Ni kweli kunachangamoto ,tusikae ofisini,tutumie muda mchache wa kusoma mafaili ,kupitia nyaraka ,lakini tukimbilie wananchi na kufanya kazi za kutatua kero zao ili Wananchi waipende Serikali yao”Bomboko
Bomboko amesema,katika Wilaya ambayo yeye ana mwakilisha Rais Samia Suluhuu Hassani,hatarajii kuona tunazoea shida za Wananchi ,
Kwa hiyo niwaombe sana Watendaji wa idara zote nilizozisema kwamba Wananchi asizoe shida ,na Mimi ni rafiki na mpenzi wa kila mmoja ambaye anasaidia kuondoka shida za Wananchi anapeleka huduma kwa Wananchi ,
Hii ni ili kutimiza adhima ya Rais Samia Suluhuu Hassani ya kuwaletea maendeleao Wananchi , Hivyo naomba ushirikiano kufikia malengo ya maendeleao.
Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Edmund Rutaraka, Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Dionis Myinga Kwa pamoja ,wamesema watashirikiana na Mkuu huyo wa Wilaya ili kufika malengo ya kuwaletea maendeleao Wananchi wa Hai
Lazaro Twange wakati wa kuaga ,alishukuru Wananchi wa Hai kwa ushirikiano walimpa na hadi kufikia hapo,nakuomba ushirikiano kama huo wauendeleza kwa Mkuu huyo mpya
Mwisho