Site icon A24TV News

DCEA KANDA YA KASKAZINI IMETEKETEZA DAWA ZA KULEVYA KILOGRAMU 185.35 ARUSHA

Na Geofrey Stephen Arusha .

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 15.01.2025 kwa niaba ya Kamishna Jenerali imeteketeza dawa za kulevya kilogramu 185.35 katika Dampo la Maji ya Chai liliopo wilayani Arumeru katika Mkoa wa Arusha.

Katika dawa hizo zilizoteketezwa, mirungi ilikuwa kilogramu 154.35 na bangi mbichi ilikuwa kilogramu 31 ambapo jumla ya watuhumiwa watano walikamatwa kwa makosa ya kupatikana na dawa hizo.

Uteketezaji wa dawa hizo umefanyika kwa kuzingatia taratibu zote za kisheria ambapo Mahakama ya Wilaya ya Arumeru iliridhia vielelezo hivyo viteketezwe kwani uwezekano wa kuleta madhara kwa binadamu ni mkubwa endapo zitaendelea kuhifadhiwa.

Zoezi hilo la uteketezaji umeshirikisha Maafisa kutoka Taasisi za Serikali akiwemo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Afisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Arusha pamoja na Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Arumeru.

*_MWISHO_*