Site icon A24TV News

Mwenyekiti akomaa kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vya ulawiti na ubakaji Bomang’ombe

Hai,

Mwenyekiti wa mtaa wa Kibaoni Bomang’ombe Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Boniphes Mrema, amesema atahitisha mkutano wa dharura wa Wazazi na walezi ili kuja kuweka mpango wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwamo ulawiti na ubakaji

Haya yamesemwa na Mwenyekiti huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo amesema anahitisha mkutano ili kupanga namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

“Ni kweli naitisha mkutano wa Wazazi na walezi kuja kuweka mpango mkakati wa nama ya kudhibiti matendo ya ukatili dhidi ya watoto ikiwamo ulawiti na ubakaji “amesema Boniphes.

Amesema amelazimika kusema hivyo,wakiwa kwenye vikao vya shule kumekuwa na taarifa ya kwamba kwenye shule zilizopo kwenye Maeneo hayo kuna changamoto zimekuwa zikiripotiwa za watoto kufanyiwa vitendo vya kulawitiwa na kubakwa

Haya mambo yamekuwa matatizo makubwa ,walimu wamekuwa wakigundua haya mambo kwa sababu muda mwingine wanakuwa na hawa watoto

Boniphes anesema, sasa shida inakuja unapotaka ushirikiano kwa jamii,kwa maana ya Wazazi inakuwa ngumu, mzazi anaweza kuelezwa tatizo kwamba mtoto wake anashida flani ,lakini hatilii mkazo anaona mtoto wake kama amezushiwa

Kwa mazingira haya yanaleta ungumu kumaliza ili tatizo ,jambo hili hali wezi kutatuliwa na mtu mmoja , wazazi hawana ushirikiano na watoto wao

Amesema kutokana na hali hiyo wameona sasa,wamejipanga kukutana na wazazi ili kuzungumza na jamii nzima kueleza hali halisi ya matukio yaliyopo na kwa namna gani kuwadhibiti

Aidha amesema kwenye vikao vingi Wazazi wachache ndiyo wanaohudhuria ,sasa tutajitahidi ili wawezo kufika kwa wingi kwenye mkutano huo amesema amesisitiza Boniphes

Baada ya kikao ya kikao na Wazazi na walezi hao tunaweza kupata njia sahihi ya kuanza kupambana na mazingira ya aina hiyo

Mbali na hilo pia ,amesema wapo kwenye operesheni ya kimiya kimiya ili kutokomeza vibaka wanaowapora Wananchi vitu mbalibali ikiwamo simu na fedha kwenye eneo hilo ili Wananchi waweze kutembea bila ya kuwa na hofu na kuishi kwa amani

Pia amesema bila ushirikiano kutoka kwa Wananchi zoezi hilo litakuwa ngumu kufanikiwa ,

Anasema ameingia kwenye uongozi kwa mara ya kwanza mtaa wa Kibaoni,hali ya mazingira na watu wake ni nzuri kwa kiasi chake

Lakini changamoto ya uwizi vibaka wanapora watu watu vitu mbali mbali ikiwamo simu na fedha,kwa kushirikiana na Askari kata tumejaribu kutengeneza mpango kazi ili kuweza kuthibiti makundi hayo ya vibaka

Kwa kiasi flani tumefanikiwa mpaka hapa tunapozungumza muda huu hali nishwari ,bado tunaendelea na operesheni ya kimiya kimiya ,hatuwezi kuona watu wanataka utajiri bila kufanya kazi

Awali wakazi wa eneo hilo akiwamo Yasin Munisi, amesema ,wamekuwa wakilalamika uwepo wa vibaka wakifanya uporaji majumbani kwa kuiba vitu mbalibali ikiwamo radio,simu , pamoja na tv , nyakati za mchana na usiku

Amesema vibaka hao wamekuwa wakitembea na vitu vyenye ncha kali ikiwamo mapanga na marungu na kutishia Wananchi nakuwapora

Mwisho