Na Bahati Hai,
Mwenyekiti wa kijijii cha Mkombozi kata ya Masama Kusini Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Julius Malya,amesema kipaumbele cha kijijii hicho baada ya uchanguzi ni kulinda vyanzo vya maji ili Wananchi wa eneo hilo waendele kufanya kilimo cha umagiliaji chenye uhakika
Kauli hiyo ameitoa alipotembea vyanzo viwili vilivyopo katika Kijijii hicho na kukuta uharibifu mkubwa ikiwamo kukatwa miti na mifugo kuingia kuingizwa katika eneo hilo jambo ambalo linaweza kusababisha vyanzo hivyo kukauka.
Akizungumza na waandishi wa habari walifika Kijijii hapo, amesema kwamba kipaumbele ni ulinzi wa vyanzo hivyo ili maji yawezo kuongezeka na Wananchi wafanye kilimo na kupata chakula ikiwamo cha biashara
“Ni kweli baada ya kuchaguliwa nimekuta vyanzo hivyo zipo hatarini kukauka ,sas kipaumbele ni ulinzi wa vyanzo hivi vya maji kwani kupitia vyanzo hivi Wananchi wanafanya kilimo cha umwagili chenye uhakika”amesema Julius,
Julius amesema katika kijijii hiki yanalimwa mazao mbalibali ikiwamo mboga za majani kama mchicha,mnavu,nyanya ,matango vitunguu maharage pamoja na mahindi na kuuzwa katika masoko mbali mbali likiwamo soko la Sadala hivyo kuwaingizia kipato Wananchi hao
Kutokana na umuhimu wa vyanzo hivyo ambavyo vikuza uchumi wa Wananchi wa eneo hili tumeona ndiyo kipaumbe itakuwa ni ulinzi wa hali ya juu wa kuhakikisha miti haikatwi na mifugo kutokuingizwa katika eneo hilo
Mbali na hilo pia amesisitiza kwa kusema kwamba kama kuna mtu ana miti mingi na anataka kuipunguza upo utaratibu wa kufuata ,kuwaona Viongozi upewe utaratibu sambamba na kupanda miti minne ndiyo aruhusiwe kukata
Baadhi ya Wananchi wa eneo hilo, wamesema Utaratibu wa kutunza mazingira huu pia ni jitihada za kuunga mkono Rais Samia Suluhuu Hassani za mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira na kurudisha uoto wa asili.
Maria Kimaro mkazi wa kijijii hicho ,amesema awali katika Kijijii hicho kulikuwa na chemi chemi za maji nyingi sana,jamii ilinufaika na kilimo cha umwagili na watu kupata mazao mengine yakiwamo ya chakula na biashara
,lakini Kadria muda unavya kwenda na watu wanaharibu mazingira,vile chemi chemi zimebaki chache , sasa hicho anachofanya Mwenyekiti tunamuunga mkono jitihada za kutunza mazingira na tunataka ziwekwe sheria na kutunza vyanzo hivyo na kufufua pia vya zamani
Mwisho