Siha,
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Paschal mboto, amesema athiri iliyokuwepo katika hospital hiyo ni Watumishi 6 walioajiriwa kutoa hudumia kwa watu wenye vvu mishahara yao ilisitishwa baada ya tangazo la Trump
Kauli hiyo imekuja baada ya Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Dancan Urasa kutaka kufahamu baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusitishwa kutoa misaada katika maeneo ya afya kuna athari yeyote imejitikeza katika Wilaya yetu
Mganga Mkuu huyo Akizungumza February 14 2025,kwenye Baraza la madiwani halmshauri hiyo, amesema athari iliyopo ya watumishi 6 mikataba kusitishwa na kukosa mishahara,wale ambao walikuwa wanalipwa na shirika la (USAID)la kimarekani
“Ni kweli mishahara yao imesitishwa ,hapo hospital ya wilaya wapo watumishi 6 kwenye hospital ,lakini wapo wengine ambao idadi yao bado sijuapata kamili takutafutia sehemu mbalibali ikiwamo vituo vya Ashengai na Ngarenairobi “amesema Paschal
Paschal amesema watumishi hao walipewa barua kwamba waondoke wasiwepo kwenye maeneo ya kazi ,mkataba wao umevunjika ,tukaona tuwabakize watusaidie wagongwa wetu kule chini majumbani wanawafuata na kuwatibu.
Tukaona tukiwaruhusu waondoke hatupata wapata wale wagonjwa watakosa matibabu na wao ndiyo wanafahamu na wamefundishwa ,
Kwa vyovyote vile idara ya Afya wale tuwaombe tukae nao ,kama watumishi wa hospital chanajichanga mwenye elfu ishirini au thelathini ,tubebane angalau waendelee kukaa na sisi kwa siku 90 yaani miezi mitatu ambazo tumekubaliana kuendelea kuwa nao
Kwa hiyo Mwenyekiti tumewabakiza waendelee kufanya kazi kwa hizo siku niaba ya halmshauri sio tena lile shirika la USAID , kuhusu dawa zipo za kutosha
Diwani wa kata ya Gararagua Zakaria Lukumai, Akizungumza amesema taarifa ni ya kusikitishwa sisi kama watanzania tunapaswa kusaidiana ,kuna watu ambao wanatumika kuwasaidia wenzetu walioathirika na ukimwi
Baada ya sitisho hilo Baraza limetoa pendekezo, Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi aweze kukaa na Mganga Mkuu wa Wilaya ipitie CMT ifike kamati ya fedha tuone namna ya kulibeba ili jukumu
“Ni kweli mapendekezo yatu Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri pamoja na Dmo ipitie CMT ifike kamati ya fedha tuone namna ya kulibeda Ili jukumu kwani ni letu”amesema Lukumai
Kwa upande wake Diwani wa viti maalumu Liliani Mollel amesema hili ni tatizo sio kwa Siha peke yake Tanzania na Dunia ni vizuri Serikali yetu hata halmshauri zetu zikawa na mafungu ya tahadhari na mafungu ya tahadhari kwa ajili ya vitu vinavyojitokeza kama hivi
Aidha Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Dancan Urasa, mara baada ya kauli hiyo amesema wamepanga kuwawezesha watumishi hao walioajiriwa kutoa hudumia wahanga wa ukimwi
Amesema kuna athiri ya kiwango kikubwa sana kama hatua hazitachukuliwa za kuhakikisha watu hawa wanabaki,kwa sababu wasipotoa zile dawa wale waathirika miili yao itaendelea kudhoofika na watu wataambukizwa kwa wingi na nguvu kazi ya Taifa itapungua
Kaimu Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Mark Masue, amesema,mpaka sasa ofisi ya Mkurungenzi haijapokea maelekezo yeyote kutoka Serikalini,wakati tuendelee na utaratibu huo,lakini tusubiri maelekezo ya Serikali
Mwisho