Na Bahati .Hai
Kukamilika kwa ujenzi wa daraja katika kitongoji cha Kibwehehe Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro limewafurahisha Wananchi kwamba litarahishisha usafirishani wa mazao kupelekea masoko mbali mbali nje ya wilaya na ndani likiwamo la Sadala
Daraja hilo lililojengwa na Shaabani Mwanga ambeye ni mdau wa maendeleao Wilayani humo , litawapunguza utoro kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wanaopita eneo hilo hasa kipindi cha masika.
Wakizungumza Junuary 3 2025,baada ya uzinduzi huo ulifanyika katika kitongoji hicho,ambapo ni kuinganishi cha vijiji vinne ,wamemshuku mwananchi huyu kwa kuona umuhimu wa kuwajengea daraja hilo.
“Ni kweli ameonyesha uzalendo kwa kujenga daraja hilo ,hii inaonyesha anatabia nzuri ya kujitolea, usipokuwa na tabia ya kujitolea hatuwezi kuacha alama, hatuwezi kuacha kitu ambacho watu watakukumbuka nacho huyu amefanya hivyo “Wamesema Wananchi hao
Sadiki Kweka mkazi wa eneo hilo , amesema muda mrefu eneo hilo limekuwa kero kwa Wananchi hasa kipindi cha mvua, kumekuwa na adha ya kutokupitiki kwa sababu hakuna daraja ,
Wakati mwingine kuwalazimu kutumia barabara nyingi yenye mzunguko mrefu hivyo kusababisha kuchelewa sehemu usika au kama ni wanafunzi wanachelewa masomo na wakati mwingine wanakuwa watoto
Amesema sasa kukamilika kwa daraja hilo umekuja wakati muafaka,mvua zikinyesha,ukimwambia mtoto nenda shule hauna shida tena unaamini kwamba daraja lipo atapita salama,ni jambo jema amefanya
Amina Munisi amesema,vijiji ambavyo vinanufaika na Daraja hilo,ni pamoja na Kijijii cha Modio,Isawara,Kimira na Mbweera,kwa ajili ya kusarisha mazao ya biashara kwenda soko la Sadala kuuza mazao na kununua kwa hiyo daraja ni muhimu sana na adha itakuwa imeondoka
Amesema kipindi cha mvua gharama za nauli zinaongezeka hasa Kwa usari wa bodaboda kutokana na mzunguko kuwa mkubwa,labda sehemu ilitakiwa ulipe sh,3000 unalazimika kutoa sh,6000 ,aliyejenga Mungu amfanyiwe wepesi katika shughuli zake
Aidha Shaabani Mwanga akizungumza swala hilo , amesema kumekuwa na kero katika eneo hilo adha Wananchi wakipita kwenda kwenye shughuli zao hivyo kuona umuhimu wa kuweka daraja hilo ili kuondoa adha hiyo kwa kushirikiana na jamii
Amesema ujenzi huo ni kumuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhuu Hassani za kuwaletea maendeleao Wananchi,kwani amejenga miradi mbalibali ya maendeleao ikiwamo vituo vya Afya, Ujenzi wa vyumba vya madaradasa, barabara,na miundombinu ya maji, katika Wilaya hii
Amesemavkuna haya madogo ambayo yapo kwenye levu ya kitongoji Wadau wa maendeleao na Wananchi tutashrikiana kama walivyoshirikiana hapo ndiyo tunawaza kusema
Awali Daud Shuma alisoma risala kuhusu ujenzi huo amesema umegharimu kiasi cha sh,4.5 million ,baada ya kumuomba mdau huyu kujenga daraja hilo,mbali na daraja pia tumemuomba afanye ukarabati wa Baraza Kwa kuweka moramo na amekubali
Mwisho