Na Bahati Siha .
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa chama cha mapindizi(CCM),Wilaya ya Siha Abdallah Chumu,amewashukuru Wadau wa michezo Wilayani humo kwa kufanikisha kwa kiasi kikubwa kumalizika kwa Ligi ya Samia Wazazi cup Siha kwa mafanikio
Kauli hiyo ameitoa February 16 2025,mara baada ya mashinda hayo kufikia ukingo katika uwanja wa ccm SanyaJuu Wilayani humo na yalianza mwaka jana,kushirikisha timu 17.
Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo wakati timu zikikabidhiwa zawadi ,amewashuru Wadau hao wa michezo kwa kuona umuhimu na jitihada za kuona michezo inasonga mbele Wilayani humo.
“Ni kweli lazima niwapa kongole wale wote waliotusaidia kufanikisha michezo hii hadi kufikia tamati leo,kwani ni kukuza michezo ndani ya Wilaya yetu na Taifa kwa ujumla na kwamba zoezi hilo ni endelevu”amesema Chumu
Amewataja walioweka mkono katika mashindano hayo kwamba ni pamoja Mkuu wa Wilaya Christopher Timbuka, Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi ambao wamekuwa nao muda mwingi
Chumu amewataja Mdau wingine aliwaunga mkuno ni pamoja Tumsifu Kweka ,ambapo amesema amewasaidia sana,lazima tuseme ukweli ametusaidia kwa kiasi kikubwa sana kuhakikisha wamefanikisha mashindano hayo.
Aidha amesema wamekumekutana na changamoto mbali mbali ya wengine kuona mashindano hayo yasifanyike lakini Mungu amesaidia yamefanyika tena kwa kiasi kikubwa
Awali Mwenyekiti wa Jumuhiya hiyo Meijo Laize,amesema lengo la mshindano hayo,yalikuwa na malengo matatu,la kwanza kuwakusanya vijana na kujielewa ili kujishughulisha na michezo
Kama unavyofahamu , sasa hivi michezo sio burudani tuu ,michezo inajenga Afya ,michezo ni ajira,pili ni kuhakikisha vijana hao wanaepuka na matumizi ya dawa za kulevya na
Amesema lengo la tatu ni kuwapa frusa vijana kuona kazi nzuri za miradi iliyofanyiwa na Rais Samia Suluhuu Hassani ikiwamo ,ujenzi wa vyumba vya Madrasa ,vituo vya Afya ,ujenzi wa barabara na miradi ya maji katika Wilaya hiyo.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza akiondoka na kitati cha sh,2 milioni pamoja na kombe na medali mahindi , mshindi wa pili sh,1 milioni na medali
Mashindi wa tatu akiondoka na shilingi laki Tano na medali na mashindi wa nne akipanda shilingi laki mbili na nusu,
Baadhi ya Wakazi wa SanyaJuu, shaabani Muhamedi,ameongeza Jumuhiya nakuomba nyingine ziendelee kuwekeza kwenye michezo kwani Wananchi wa Siha wanapenda michezo
Kwa upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi ambeye alikuwa mgeni rasmi,awapo kongole Jumuiya hiyo kwa na maono kwa kuandaa kitu hicho ambacho kinakuza michezo Wilayani humo
Mwisho