Site icon A24TV News

DPP AMSOMEA MASHTAKA 60 YA UJUMU UCHUMI MFANYA BIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA! MAWAKILI WANENA MAZITO KUHUSU KESI HIYO

Na Geofrey Stephen Arusha .
SERIKALI imemsomea mashtaka 60 ya uhujumu uchumi ,mfanyabiashara na mwekezaji Saleh Salimu Alamry (54) Mkazi wa Njiro Jijini Arusha akikabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu, kughushi na utakatishaji fedha haramu kiasi cha dola za kimarekani milioni 8 akiwa mkurugenzi mwenza wa kampuni mbili za uwindaji na utalii ya Sunset Tarangire limited na AIrajhi Holdings LTD.
Mwingine aliyesomewa mashtaka ni wakili wa kujitengemea Sheck Mfinanga ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo.
Akisoma mashtaka hayo leo februari 20,2025  mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya  hakimu Mkazi Arusha,Erasto Philly ,wakili wa  serikali mwandamizi,Edgar Batulaki  akisaidiana na Jackline Mosha na Alawi  Miraji,alisema agosti mwaka jana walipata  malalamiko kutoka kwa wabia  wenzake Khaled Alrajhi na Abdulkarim  Alrajhi raia wa nchi ya Saud Arabia.  
Wakili alisema kuwa wabia wenzake kupitia  kampuni yao ya Sunset Tarangire limited na  Alrajhi Holdings LTD walidai kuwa Saleh  Amry ambaye ni mkurugenzi mwenza  alifanya vitendo vya uhalifu kwa kupoka hisa  18 isivyo halali ikiwa ni mali ya kampuni hizo  na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Alisema mwekezaji huyo na wakili mfinanga  walikamatwa na uchunguzi ulifanyika na leo  uchunguzi umekamilika na mahakama ya  hakimu mkazi imefunga mashtaka ,na  mashtaka yao yataenda kusikilizwa na  mahakama kuu kitengo cha rushwa na  uhujumu uchumi kwa makosa yote 60.
Wakili Batulaki alisema kuwa matukio hayo  yalifanyika kati ya mwaka 2019 hadi 2024 na  waliyatenda katika mikoa ya Arusha,Dar es  Salaam,Pwani na Manyara
Aliieleza mahakama hiyo kuwa ofisi yake  imejipanga na kesi hiyo na imejianda kule a  Mashahidi 80,vielelezo 461
Akiongea nje ya mahakama wakili  anayemtetea mshtakiwa wa kwanza Mosses  Mahuna na Faisal Rukaka alisema  kikichofanyika leo mahakamani hapo ni  kufunga shauri hilo baada ya washtakiwa  kusomewa mashtaka yao na kesi hiyo  kuhamishiwa mahakama kuu kitengo cha  rushwa na uhujumu uchumi ambayo ndio ina  mamlaka ya kusikiliza shauri hilo,
Alisema wao wamejipanga na utetezi wa  mteja wao na wanasubiri shauri hilo  lipangiwe tarehe ya kuanza kusikilizwa  katika mahakama kuu kitengo cha mafisadi.
Mwisho .