Na Geofrey Stephen Arusha .
Miradi hii, yenye ufadhili wa EUR milioni 8 kutoka EU, inalenga kuondoa vikwazo vya biashara, kuimarisha utekelezaji wa sheria za ushindani, na kuongeza uwezo wa taasisi za EAC, huku ikitoa msukumo maalum kwa uwezeshaji wa wanawake na vijana.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Forodha, Biashara na Masuala ya Fedha, Bi. Annette Ssemuwemba Mutaawe, alieleza shukrani zake kwa EU kwa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya EAC.
Annette Ssemuwemba Mutaawe. Katibu Mkuu wa EAC .
Kwa upande wake, Mkuu wa Ushirikiano, Ofisi ya EU kwa Tanzania na EAC.Jose-Luis Gonzalez..Meneja Program EU.
Jose-Luis Gonzalez..Meneja Program EU.
alisema miradi hii ni sehemu ya mkakati wa EU wa kusaidia muungano wa kikanda kupitia Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) na Mpango wa Team Europe, kwa lengo la kujenga uchumi thabiti na jumuishi zaidi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na maafisa wa ngazi ya juu kutoka EU na EAC, washirika wa maendeleo, pamoja na wawakilishi wa sekta binafsi na mashirika ya kiraia.
Mwisho .