Site icon A24TV News

WANAFUNZI MSIWE MABUBU KATIKA VITENDO VYA ULAWITI ,UBAKAJI MPAZE SAUTI .

Na Bahati Siha,

Mkuu wa shule ya Sekondari Ormelili Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Hapriday Msomba ,amewataka wanafunzi wa shule hiyo wasiwe mabubu katika elimu waliweyo pewa ya kujilinda dhidi ya ukatili wa kijinsia ikiwamo ubakaji na ulawiti

Haya yamesemwa na mwalimu huyo wakati wa Kampeni ya msaada wa kisheria ijulikanayo kwa jina la kampeni ya mama Samia legal Aid ,ilipotembelea shule hiyo,na kuzungumza na wanafunzi kuhusu changamoto zinazowakabili pia kuwajengea uwezo wa kupambana dhidi ya matendo ya ukatili.

Mkuu huyu wa shule Akizungumza mara baada ya elimu hiyo,alishukuru kitengo hicho na kuwataka wanafunzi wasiwe mabubu na waendelee walawafundishe wengine

“Ni kweli msiwe mabubu,hichi mlichokipata hapa mkawa elimishe hata wadogo zenu , Wazazi msiwagope ,wambie baba shuleni wamekuja Wageni wametufundisha moja mbili tatu

Msomba amesema hii elimu ya ukatili mkieneza uko ,itafika wakati haya mambo yataisha Kwa sababu watu wamepata elimu na wemeelimika.

Amesema wa sasa kila kukicha utasikia kwenye vyombo vya habari aarifa za ukatili ,sasa kwa hii timu ya msaada wa kisheria ya mama Samia imefika wakati muafaka itatusaidia Kwa watoto wetu

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo akiwamo Godlight Mollel ,moja ya amesema kwamba ukatili mwingine uliopo katika maeneo hayo ni ndoa za utoto kwa watoto wa kike na watoto wadogo wa kiume kutumikishwa kuchunga mifugo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu

“Ni kweli kuna mabinti wadogo wanaozeshwa baadhi ya wanafunzi hasa eneo hili la wafugaji mwanafunzi akishindwa mtihani wa kidato cha pili wanamuozesha hapana ,tusonesheni ili kujakupata wasomi kwenye Taifa hili”amesema Mollel.

Awali Afisa ustawi wa jamii Wilayani humo Peter Msaka, amesema vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ikiwamo ubakaji na ulawiti kuongezeka hivyo kuwataka watoto kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuzingatia somo walilopewa

Amesema somo hilo ni pamoja wanapoona viashiria vya kufanyiwa ukatili ,wakimbie,au wapige kelele kuomba msaada kwa watu.

Pia watoe taarifa kwa watu wanaowaamini ikiwamo kwa Wazazi, Viongozi wa Dini , Viongozi wa Serikali ,pamoja na walimu shuleni hili ni katika jitihada za kukabiliana na vitendo hivyo na watoto wabaki salama

Mwisho