Site icon A24TV News

Wananchi siha waomba kampeni ya Mama Samia ya msaada wa kisheria kuweka kambi ya kudumu Wilayani humo

Siha,

Wananchi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wameomba kampeni ya mama Samia ya msaada wa kisheria kuongoza muda ndani ya Wilaya hiyo na kuendelea kutoa huduma hiyo kwani changamoto za Wananchi ni endelevu ikiwamo migogoro ya aridhi, ndoa na mirathi

Hatua hiyo imekuwa baada ya muda walipewa wasaidizi hao kutoa huduma kufikia mwisho February 8 2025 uku Wananchi wakionekana bado wanauhitaji.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti , wamemuomba wasaidizi hao waweke kambi ya kudumu kwani changamoto kila siku zinajitokeza

“Ni kweli kila siku matatizo ya Wananchi kila siku yanajitokeza hivyo wasaidizi hao walitupa mwanga wa sehemu ya kuanzia , sasa wamemaliza kampeni yao Wananchi watarudi kule kule ya kupoteza haki zao,ndiyo sababu ya kuomba waweke kambi”wamesema Wananchi hao

Idrisa Mndeme mmoja ya Wananchi hao mkazi wa SanyaJuu, amesema kwamba katika mkoa huu wa Kilimanjaro kesi nyingi ikiwamo migogoro ya Aridhi ndoa,unyanyasaji wa kijinsia pamoja na mirathi,

Idrisa anasema ilipofika hii kampeni ya Mama Samia ya msaada huo wa kisheria watu wengi hasa wenye kipato cha chini walijitokeza kutoa malalamiko yao ambapo walipata elimu hiyo kwenda kuzifanyia kazi.

Sasa muda wao ulifikika mwisho February 8 2025, wakati Wananchi bado wanauhitaji na hata kuna baadhi ya sehemu hawakufika, tunaomba waweke kituo cha kudumu ili waendelee kutoa huduma kwa Wananchi

Amesema msaada wa elimu hiyo ikiendelea kutolewa itapunguza msongamano wa kesi mahakamani na itapunguza vifungo vya watu ambao wasio sheria,Tunashukuru Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kuliona ili kwani Wananchi wengi watapata Mwanga wa kujua haki ndiyo sababu ya kuomba muda uongezwe.

 

Kwa upande wake Jocob Kiruswa mkazi wa Kijijii cha Sinai, amesema amepata elimu kuhusu umuhimu wa kuweka utaratibu mzuri wa kugawa mirathi ili bada ya mtu kufariki kusitokee ugomvi wa kugombea mali

“Ni kweli leo nimejifunza namna bora ya utaratibu wa mirathi ili kuzuia ukatili wa baadaye inaweza kujitokeza wa kugombea mali zilizoachwa na marehemu “amesema

Humphrey lyapa Afisa Dawati la msaada wa kisheria halmshauri hiyo ya Siha,ambeye inaratibiwa na kampeni ya Mama Samia ya legal Aid, amesema kampeni hiyo Wilayani humo ilizinduliwa Junuary 30 2025 na kumalizika February 8 2025, bado itaendelea kutolewa hapo halmshauri ya siha.

 

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kutatua changamoto ambazo zinawakabili Wananchi katika maswala mbalibali ikiwamo migogoro ya Aridhi,ndoa, mirathi,makosa ya jinai, madai,pamoja na ukatili wa kijinsia, msaada ambao ni bure

Niwatoe wasiwasi Wananchi kwamba huduma bado inaendelea kutolewa na maafisa ambao wanapatikana halmshauri hiyo ya Siha,Kwa hiyo Wananchi atakaye kuwa na changamoto ajitokeza katika ofisi hizo hapo halmshauri

Mwisho