Siha,
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT),Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Idrisa Mndeme ,amesisitiza Wananchi kata ya SanyaJuu ,kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo yao kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya uhalifu
Ametoa kauli hiyo February 18 2025, kutoka wezi kuongezeka ikiwamo wa fedha maduka kadhaa ya bidhaa eneo la Sanya juu yakiwamo ya nguo kuvunjwa na kuibiwa na watu wanaodaiwa ni vibaka
Akizungumza na waandishi wa habari, ametoa rai kuundwa kwa vikundi na kwamba jukumu la usalama wa Wananchi sio la jeshi la Polisi pekee,
“Ni kweli jukumu la usalama wa Wananchi sio la Jeshi la Polisi pekee,hivyo uwepo wa vikundi vya ulinzi shirikishi ni muhimu “amesema Idrisa
Idrisa amesema Viongozi wa vijiji na kata wanapaswa kushirikiana na Polisi kata kuunda vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi kwa ajili ya kukabiliana na wahalifu ili Wananchi waweze kuwa salama
Na kuendelea na shughuli zao za maendeleao bila kusumbuliwa na wahalifu
Lazima kuhakikisha Wananchi wanaishi kwa amani na utulivu ,kwa sababu haiwezekani mtu ametafuta mali yake kwa jasho alfu badala ya kupumzika usiku anakaa macho kwa ajili ya kuhofia kuibiwa mali hii haiko sawa
Kwa upande wake mkazi wa SanyaJuu Wilayani hapa, Joyce Mmari amesema kutokana na ongezeko wizi mdogo mdogo kwenye maeneo ya wafanyabishar na maeneo mengine ya nyumbani kuna sababisha maendeleao kurudi nyuma
Hivyo ni wajibu wa Viongozi wetu kuliona hilo la kuanzishwa vikundi ili kuzuia na kudhibiti uhalifu
Pia jambo kingine la kufanya kunaitajika kwanza walinzi ambao wanalinda katika maeneo ya maduka kuwa na taarifa ya maeneo wanapotoka
Wafanyabishar wahakikishe kwenye biashara zao zinakaa katika mfumo wa ulinzi,kwa sababu Askari wa Jeshi la Polisi ni wachache,hawa wezi kupiga doria usiku kucha katika eneo moja
Mwenyekiti wa kijijii hicho cha SanyaJuu Wema Gasino, Akizungumza swala hilo ,amesema watafanya kikao ili kujadili namna bora ya ulinzi
Mwisho