Site icon A24TV News

Dc Bomboko akerwa na uchafu kituo cha mabasi Bomang’ombe pamoja na soko la walaji

Hai,

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Hassani Bomboko,amewataka maafisa mazingira Wilayani humo kuhakikisha wanasimamia wajibu wao ili mazingira yao safi hasa ,kipindi hiki cha mvua ili kuepuka magonjwa ya mlipuko ikiwamo kipindi pindu

Hatua hiyo imekuja baada ya kufanya ziara ya kustukiza katika kituo cha mabasi na Bomang’ombe na soko la walaji na kukuta kadhia ya mrundikano wa uchafu wa aina mbali mbali ikiwamo, maji kutuama na kutoa harufu

Akizungumza na wafanyabiasha wa soko la hilo, amewaambia amewataka maafisa hao wa mazingira kuacha kukaa ofisi ,watoke nje na kwenda kutimiza maswala ya usafi kwa jamii.

“Ni kweli nimefika hapa kituo mabasi Bomang’ombe pamoja na soko hili kusikiliza kero zilizopo hapo na kuzitatua, lakini kabla ya kuja hapa nimetembea maeneo mengi ni machafu”amesema Bomboko

Bomboko amesema baada ya kupata taarifa kwa wasamaria wema ya uwepo wa uchafu katika maeneo hayo ,hakutaka kumjulisha mtu yeyote na kuamua kufanya ziara ya kustukiza, matokeo yake ndiyo kama tulivyona

Mara baada ya kufika na kutembelea kituo cha mabasi Bomang’ombe,akiwa ameongozana Mkurungenzi Mtendaji wa halmshaur, na Watendaji wangine wakiwamo maafisa mazingira

Walishuhudia mrundika wa uchafu ulikaa muda mrefu ,mifereji kutuamisha maji machafu na kusababisha harufu mbaya, makopo kutupwa hivyo jambo ambalo sio sahihi mbapo pia walitembea kwenye soko hili la walaji changamoto zikiwa hazina tofauti sana na walizokuta stend

Bomboko baada ya kutembea maeneo hayo, aliomba kuitiwa wafanyabiasha wa maeneo hayo ili kuongea na kusikiliza kero zao

Flora Mtui, mmoja ya wafanyabiasha wa soko ilo amesema miundombinu ya choo sio mizuri ,maji yanakatika hovyo na kusababisha kukosekana katika choo cha soko hilo ,jambo ambalo linasababisha kero kubwa kwa wananch

Flora amesema pia miundombinu ya choo sio mizuri, vyumba viwili tuu vya choo ndiyo vinafunguliwa vingine vimefungwa na watu ni wengi wanafika kujisaidia, ukifika unasubiri haja inaweza kutoka wakati unasubiria ,wafanye ukarabati na kufungua hivyo vingine

John Swai is Mganga biashara wa eneo hilo Lalamiko lake liingine lililotajwa hapo ni biashara ya pombe haramu ya gongo kufanyiwa katika soko hilo

Kero nyingine baadhi ya vizimba kuvuja mvua inaponyesha,baadhi kukosekana taa ,mitaro kuziba kutopitisha maji, mrundikano wa uchafu

Mara baada ya kusikiliza kero hizo Mkuu huyo wa Wilaya, amewataka maafisa mazingira kuhakikisha miundombinu ya soko inakuwa sawa ili Wananchi wafanyabiasha kwa amani na utulivu ,hata wezi kuwa na ctendi chafu hapana

Tumetembea tumeona na pia wafanyabiasha wasema hapo miundombinu sio mizuri kituo cha mabasi Bomang’ombe pamoja na sokoni la walaji,rekebisheni miundombinu ili watu wafanya shughuli zao kenye maeneo safi”amesema Bomboko

Bomboko amesema amepokea kero 9 ikiwamo ya choo kukosa Maji na kuwataka watu wa mazingira kuhakikisheni maji yanapatikana,koki vinafungwa ,taa sehemu ambazo hazipo zinawekwa watu waweze kufanya biashara hadi usiku

Pia Mitaro ya maji ya nje iliyojaa hakikisheni inatoka pale ,hasa kipindi hiki cha mvua za masika ni hatari kunaweza kutokea magonjwa ya mlipuko ,msikimbilie kukaa ofisi tokeni mtembelee maeneo yenu ya kazi

Wafanyabiasha hao wamempongeza Mkuu wa Wilaya Kwa kuona umuhimu wa kuwatembelea na kusikiliza kero zinazowakabili

Mwisho