Site icon A24TV News

 Dc hai Hassani Bomboko,aunda timu ya kufutilia mgogoro wa Aridhi Kijijii cha mkombozi Wilayani humo

Na Bahati Hai,

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Hassani Bomboko,ameunda timu ya kufutilia mgogoro wa Aridhi kati ya Wananchi wa Kijijii cha mkombozi na baadhi ya watu wanaoudaiwa kuvamia eneo liliotengwa la kijijii hicho

Hatua hiyo imekuja baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili zinazojiushisha na mzozo huo za walalamikaji na walalamikiwa ,uku akitoa angalizo la watu kusema ukweli ili haki iweze kutendeke bila kumuonea mtu.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa dharura uliofanyika katika kijijii hicho karibu na shule mpya ya Sekondari Mkombozi na kuhudhuriwa na baadhi ya madiwani amesema timu hiyo itafutilia na kutoa majibu ya nani mwenye haki

“Ni kweli mgogoro ni ambao Wananchi wa kijijii hiki walilalamika nilipokuja kukagua Majengo ya shule hii ya mkombozi, na leo nimekuja kusikiliza ,na ili kuweza kumaliza kero hii,kikubwa nachotaka ni watu kusema ukweli ili tuweze kutoa haki”amesisitiza Bomboko.

Bomboko amesema,maamuzi ambayo wamefikia kutatua moja kuhusu mgogoro huu ni kuunda timu maalumu itakayokuwa na watu kutoka idara tofauti tofauti,

Amesema kamati hiyo itakuwa na maafisa Aridhi,watu kutoka Takukuru,maafisa kutoka ofisini ya mkuu wa Wilaya watakaofanya kazi kwa njia tofauti,

Aidha amesema kamati hii itakuwa na jukumu la kupima eneo zima lenye mgogoro linabukubwa wa kiasi ganiJambo la kwanza kwenye usuluhishi ni kuwepo kwa nyaraka

Nataka kuwahakikishia hakuna haki itajayopotea ya mtu ,kama ni kijijii una haki yako utapata, hayo ndiyo maelekezo ya Samia Suluhuu Hassani kuhakikisha inatolewa haki kwa wananchi wote iwe ni raia

Amesema kwa wakati tulionao maeneo yote yenye mgogoro hayatakiwi kuendelezwa ,mpaka mtakapo niletea taarifa na mimi tafika hapo ,tapita na kamati yangu mguu kwa mguu na siku hiyo tutaitumia hapa.

Awali Mwenyekiti wa kijijii hicho Julius Malya amesema,alipoingia Madarakani hivi karibuni alipitia baadhi ya nyaraka nakuona kuna maeneo ya kijijii yakiwamo ya shule ya msingi yamechuliwa kinyemela na baadhi ya watu bila utaratibu wa kisheria hivyo kutaka kuyarudisha

Mwisho