Site icon A24TV News

PSSSF YASAINI MKATABA NA AICC UJENZI WA UKUMBI WA KISASA WA MIKUTANO MOUNT KILIMANJARO

Na Geofrey Stephen Arusha
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa  Umma (PSSSF) na Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha Arusha (AICC) zimetiliana saini ya  utekelezaji wa mpango mahususi wa ujenzi wa  ukumbi mkubwa wa kisasa wa Mikutano wa Mt  Kilimanjaro(KMICC)jijini Arusha, yakiwa ni  maono ya Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere  na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Hayo yameshuhudiwa na Waziri wa Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi  Mahmoud Thabit Kombo ,wakati wa hafla ya  uwekaji saini wa Ukumbi huo utakao kuwa na  uwezo wa kuchukua watu 5000 kwa mkupuo  mmoja.  
 “Rais Samia ameona kwa uono mpana  kabisa kuna fursa nyingi katika utalii wa  vikao, incentives, mikutano na maonesho  (meetings, incentives, conferences and  exhibition-MICE) ambazo hazijatumiwa  vizuri kutokana na miundombinu duni”
ujenzi wa ukumbi huu ambapo  ameelekeza pia ijengwe na hoteli  isiyopungua vyumba 500 pembezoni mwa  ukumbi ni mwendelezo wa Serikali yake wa  kutatua changamoto katika sekta ya  utalii”, Balozi Kombo alisema.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi  mbalimbali waandamizi wa Serikali, Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kazi vijana, ajira na  wenye ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb)  ametoa wito kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii  PSSF na AICC kuhakikisha wanasimamia vyema  mradi wa ujenzi wa ukumbi huo utakao kuwa na  uwezo wa kubeba watu 5,000 kwa mara moja.
Alisema mchakato wa ujenzi wa kituo hicho ni  matokeo ya miongozo mbalimbali  inayoongozwa na dira ya taifa ya maendeleo ya  mwaka 2025.
Utekelezaji huu ni maelekezo ya ilani  ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya  mwaka 2020 hadi 2025 inayotuelekeza  kujenga ukumbi mkubwa wa mikutano  utakaoweza kuileta Dunia Tanzania”,  Alisema.
Aidha, alisema anafarijika kuona taasisi ya PSSF  ilivyoingia makubaliano mazuri na kituo cha  Mikutano cha AlCC katika utekelezaji wa mradi  huu ambao unatakiwa kukamilika katika  kipindi cha miaka miwili.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya  Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye  Ulemavu, pamoja na kumpongeza Mhe. Rais  kwa kutoa ruksa ya ujenzi wa kituo hicho,  aliikumbusha hadhira kuwa ujenzi wake ni  maelekezo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya  Mwaka 2025 inayoelekeza umuhimu wa kujenga  mazingira wezeshi na muhimu kwa ustawi wa  Taifa kiuchumi, kijamii na kiutamaduni pamoja  na Maelekezo ya llani ya Uchaguzi ya Chamd  Tawala (CCM) ya mwaka 2021:  
Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Msajiri wa  Hazina, Bi. Neema Musomba alisema, “Msajili  wa Hazina anapongeza ushirikiano wa PSSSF na  AICC, na kuwa ofisi ya Msajili wa Hazina wakati  wowote itakuwa tayari kuhakikisha mradi huu  unafanikiwa.
Watendaji wakuu wa PSSSF na AlCC kwa nyakati  tofauti walisisitiza kutimiza wajibu wao ili  kuhakikisha mradi huokimkakati unakamilika  kama ilivyopangwa.
Mwisho .