Arusha
Katika jitihada za kuimarisha mazingira ya biashara na kukuza shughuli za ujasiriamali nchini, taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) imezindua mtandao wa kuwaunganisha wafanyabiashara na fursa
mbalimbali za kiuchumi katika ndani na nje ya nchi.
Mtandao huo unaojulikana kama KLI Alumni Connect utawahusisha zaidi ya
wafanyabiashara 300 waliopitia programu za uongozi wa Biashara na
ujasiriamali katika kipindi cha miaka mitatu kilichoendeshwa na KLNT.
kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Regent kilichoko nchini Marekani chini ya kituo cha kibiashara cha Business Development center (BDC) Tanzania cha hapa nchini katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma and Arusha.
KLNT ni taasisi inayolenga kuandaa, kulea na kuimarisha viongozi
waadilifu katika sekta mbalimbali nchini Tanzania na kuwajengea uwezo
wafanyabiashara,wajasiriamali, na viongozi wa sekta tofauti ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jana jijini Arusha,Mwenyekiti Mtendaji wa KLNT, Isaac Mpatwa amesema mtandao huo unalenga
kuunganisha wahitimu wa programu hizo na fursa mbalimbali zinazowawezesha kukuza na kuimarisha biashara zao.
“Kupitia KLI Alumni Connect, tunawapa wahitimu wetu fursa ya
kuunganishwa na ekosistemu ya biashara, mabenki, taasisi za maendeleo
ya teknolojia, na wadau wa ndani na nje ya nchi kwa zaidi ya mataifa
100 duniani tulizo na mahusiano nazo”.
Amesema hiyo itawawezesha kupata Elimu zaidi, mitaji, ubunifu,
teknolojia, vifaa, na masoko ya kimataifa.
Amesema mafunzo hayo yanaenda sambamba na safari za nchi mbalimbali
ikiwemo Israel ambapo wanarajia kuhudhuria jukwaa la Biashara na
uwekezaji linalojulikana kama ‘Tanzania-Israel Business and Investment
Forum [TIBIF] ’litakalofanyika kuanzia juni 8 hadi 14, 2025 Tel Aviv.
Jukwaa hilo muhimu la Biashara na uwekezaji, Mpatwa amesema kuwa
wameandaa kwa lengo la kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa Tanzania na Israel kwa madhumuni ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara.
“Tunawapeleka wafanyakabiashara wetu nchini Israel ili kuwaunganisha
na masoko, miradi, mitaji, fedha, mafunzo, na ushauri wa kibiashara katika sekta mbalimbali kama elimu, ufugaji, uvuvi, viwanda,
teknolojia na utalii” amesema na kuongeza
“ Tunataka wafanyabiashara wetu wapate nafasi ya kukutana na wenzao wa Israel kupitia mikutano midogo midogo ya kibiashara ‘Business tor
Business Meeting[B2B]’ iliwaweze kufaidika na fursa za biashara
zinazofanana na wenzao”
Mpatwa amesema kuwa hayo yote yanafanyika kwa ushirikiano na serikali
chini ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Wizara ya Viwanda na
Biashara, Wizara ya Uwekezaji, na Wizara ya Mambo ya Nje.
“Ushirikiano huu unalenga kubadilishana maarifa, miradi, na uzoefu
kati ya sekta ya umma na binafsi ili kuhakikisha wafanyabiashara wetu
wanaungwa mkono na mifumo rasmi ya kiuchumi na unatoa fursa za
kufanikisha makubaliano ya kibiashara kati ya wafanyabiashara na
serikali, au serikali za nchi washirika na nchi yetu.
Mmoja wa wafanyabiashara wahitimu katika programme hiyo, Rephrine Kombe amesema mafunzo hayo ya wiki 20 yamewasaidia kuwapa ujasiri wa kuwasilisha mawazo yao na kuboreshwa na wataalamu hao wa biashara na
kuwasaidia kuanza safari rasmi ya kibiashara.
“Mimi nilikuwa na wazo tayari, hivyo nikasaidiwa kuboresha nawakufunzi wetu ambao ni maprofesa wa biashara, na sasa nimefanikiwa
kuwa na biashara halisi, na zaidi nimefanikiwa kuingia kwenye mfumo rasmi wa kiserikali” amesema Rephrine ambae ni Mkurugenzi wa kiwanda
cha kutengeneza taulo za kike cha Reepads’ .
Aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Programe hiyo, Meya wa jiji
la Arusha Maximmilian Iranghe amesema kuwa elimu hiyo ya ujasiriamali
ya vitendo ni nzuri ambayo inasaidia pia serikali kukuza ajira na kukua kiuchumi kwa jamii.
“Kadri wananchi wake wanavyokua na uchumi mzuri ndivyo na serikali
inavyozidi kukua hivyo niwapongeze sana KLNT na niseme kuwa serikali
itaendelea kuwaunga mkono wafanyabiashara na wajasiriamali wote nchini
hasa katika kutatua changamoto zao wanazokumbana nazo ili kukuza biashara zao”.
Pia amewataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanatumia fursa ya uwekezaji wa nyumba za wageni ili kuchangamkia fursa ya utalii inayozidi kukua kila kukicha huku changamoto kubwa ikiwa malazi.
“Tena uwekezaji huo muanze sasa hivi maana mwaka 2027 kuna utalii
mkubwa wa mikutano na wa michezo ambazo tutakuwa na mkutano mkubwa wa wadau na wataalamu wa nyuki duniani watakaokutana Arusha unaojulikana
kama ‘Apimondia’ lakini pia michuano ya Afrika ‘Afcon’ hivyo changamkeni hela zinakuja” amesema Meya huyo.
Mwisho.