Site icon A24TV News

Baraza la Madiwani Siha la mpongeza Ded Siha na timu yake kwa ukusanyaji mapato na kufikia asilimia 98

Siha,

Baraza la Madiwani halmshauri ya Siha mkoani Kilimanjaro limempa pongenzi Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi kwa kazi nzuri ya ukusanyaji mapato

Haya yapo katika taarifa yake iliyotolewa Dancani Urasa Mwenyekiti wa halmshauri kwenye Baraza la kawaida la Madiwani ,taarifa ya kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025, ambayo inajumuhisha mambo mbali mbali

Katika taarifa yake hiyo kwenye kikao hicho kilichofanyoka katika ukumbi wa halmshauri hiyo, amesema kwa sasa wamefikia asilimia 98 ya ukusanyaji mapato.

“Ni kweli tunampo kongole kwa jitihada hizi na pia kwa kushirikiana na timu yake , waendelee na juhudi hizo ili kuleta maendeleao kwa Wananchi wa Siha”amesema Dancani

Amesema kukusanya mapato ni kazi moja , naomba kazi hii nzuri iendelee kufanyika katika matumizi ya mapato haya ili kuleta tija na malengo yaliyokusudiwa ya utoaji wa huduma katika jamii yetu

Aidha amemtaka Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo kuendelea kuweka nguvu zaidi ufuatiliaji na ukamishaji wa miradi mikubwa inayoendelea kujengwa katika halmshauri hiyo kabla ya June 30 2025 kwa mafundi waliopewa ili ikamilike kwa wakati.

ikiwamo shule ya ufundi ya Sekondari ya mkoa inayojengwa kata ya lndument zaidi ya sh,6.1 billion Shule ya Sekondari kata ya miti mirefu zaidi ya sh,5.8 milioni, pamoja na ujenzi wa zahati ya lawate sh,600 milioni

Katika taarifa yake amesisitiza swala la utunzaji mazingira kufanya usafi katika maeneo yetu, kupanda miti ikiwamo ya matunda na mbao ili kuwa na mazingira mzuri

Pia kuchuliwa kwa hatua stahiki wale wote wanaokata miti bila kufuata utaratibu na wale wanaolima kenye vyanzo vya maji ,kwani wanarudisha jidihada za Rais Samia Suluhuu Hassani za utunzaji mazingira

Aidha amewataka Tarura waweze kurejesha mawasiliano ya barabara na vivuko ili Wananchi na wanafunzi waendelee na shughuli zao za kila siku za kujiletea maendeleao,pamoja na wanafunzi kuendelea na masomo

Sambamba na hilo amewataka wazazi na walezi kuchukua tahadhari kwa Watoto kucheza sehemu karibu na maji hasa mashino na madibwi hasa kipindi hiki cha mvua za masika ili kuzuia janga kutokea

Pia amesema mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu katika Wilaya hiyo,utapokelwa julay 3 ,2025 , katika kata ya Indument ukitokea Wilayani Rombo, ujumbe wa Mwenge mwaka huu jitokezeni kushiriki uchanguzi mkuu 2025 kwa amani na utulivu.

Kwa upande wake Juma Jani Diwani wa kata ya SanyaJuu,ameoiomba Tarura Wilayani humo, kuangalia barabara amembazo hazipitiki kutokana na mvua zilipo kwenye kata yake na kuzifanyia kazi

Mwisho