Site icon A24TV News

DC HAI BOMBOKO AWATA VIONGZI KUACHA TABIA YA KUKAA , OFISINI NENDENI KWA WANANCHI MTATUE KERO

Hai,

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Hassani Bomboko,ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya watumishi kushinda ofisini badala ya kutoka nje kwenda kuwahudumia Wananchi ambao wanachangamoto nyingi zikiwamo zinazokwamisha jitihada za maendeleao

Haya yamejiri leo kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi ya mtaa wa kibaoni Bomang’ombe Wilayani humo,uliolenga mazungumza na Wananchi pamoja na kusiliza kero uliokuwa makhususi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo,uliofanyika katika ofisi ya mtaa wa Kibaoni,ameonyesha kukerwa na watumishi wenye tabia za kujifungia maofisini uku changamoto zikiwa ngingi kwa Wananchi

“Tutoke ofisini ,tutoke kwenye magari ,sisi sisi watumishi na Watendaji wa Serikali hatutopimwa kwa kukaa ofisini kwenye kiyoyozi huku tumekaa tuu, wakati Wananchi wanakero, nyingi kama mlivyozisikia hapo ikiwamo za mrundikano wa takataka hapa Bomang’ombe “amesema Bomboko

Bomboko amesema watumishi watapimwa kwa huduma wanazozitoa kwa Wananchi na kwa namna kero za Wananchi zinavyotatuliwa,nilazima tutoke tukawahudumie Wananchi wetu

Amesema leo Mkuu wa Wilaya akienda sehemu akaambiwa kuna takataka mahala ,naanza na pale yule ambaye anatakiwa kufanya kazi hiyo katika eneo hilo

Haiwezekani wewe ni Bibi afya haupiti kwenye maeneo yako ya kazi , wewe ni mtu wa mazingira haupiti unategemea nani aje afanye kazi hiyo ,mpaka linakuja kuzungunzwa kwenye mkutano hapo wa Wananchi.

Kero nyingi kutoka kwa Wananchi nazisikia ,kuna nyingine kama watumishi walikuwa wanawatembelea au kuwa karibu na Wananchi zingetatuliwa siku nyingine,lakini Wananchi wamekaa nazo hadi Leo ndiyo zinakuja kusemwa hapa,haipendezi

“Ni kweli nimesikia kero zaidi ya 15 ikiwamo maji kutuama kenye makazi ya watu , mrundikano wa uchafu ukiangalia zilipaswa kutatuliwa na kabla ya Mimi kufika hapa “amesema Bomboko

Rais Samia Suluhuu Hassani ni muadilifu ,muaminifu na mchapakazi ,sisi wawakilishi na wasaidizi wake ni lazima tuhakisi hali yake ya uchapa kazi na uadilifu wake

Kwa hiyo wenzangu wa chini , lazima muelewe huu ndiyo muelekeo. Wetu wa Serikali kwa sasa na siyo vinginevyo.

Diwani wa kata hiyo Evord Njau,amemshukuru Rais Samia Suluhuu Hassani,kwa kutoa fedha nyingi za ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleao katika kata hiyo , ikiwamo miundombinu ya maji,barabara, vyumba vya madarasa pamoja na Afya,t

Hivyo hatuna budi ya kusema asante kwa kujali Wananchi wa eneo hilo kwa miradi hiyo pamoja na Mbunge wa Jimbo ili Saashisha Mafuwe Mungu awajalie

Mwisho.