Site icon A24TV News

MKUTANO MKUU WA WANAHISA WA CRDB WA 30 NI HISTORIA KUGUSA JAMII WANAHISA KUCHEKELEA ONGEZEKO

Na Geofrey Stephen Arusha .

Benki ya CRDB leo imefanya mkutano na waandishi wa habari Jijini Arusha Wenye lengo la kuwakaribisha Wanahisa kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa utakaofanyika Jumamosi, tarehe 17 Mei 2025, katika ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha pamoja na kwa njia ya mtandao kwa wale watakao shindwa kufika ukumbini .

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dkt. Ally Laay, amesema kuwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa utafanyika siku moja baada ya Semina Maalum ya Wanahisa itakayofanyika lijumaa, tarehe 16 Mei 2025. Semina hiyo itafunguliwa rasmi na mgeni rasmi anayetegemewa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela, amewahamasisha wanahisa kuhudhuria Semina na Mkutano Mkuu,

akisisitiza kuwa ni haki yao ya msingi na ya kisheria. Pia alieleza kuwa ushiriki wao unachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza ufanisi, uwazi, na uwajibikaji katika uendeshaji wa Benki.

Mwaka huu Mutano Mkuu wa Wanahisa unafanyika katika kipindi maalum ambapo Benki ya CRDB inasherehekea miaka 30 tangu kuanzishwa kwake. Maadhimisho haya yanatoa fursa ya kutafakari mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho, ikiwa ni pamoja na kupanua huduma zake ndani na nje ya nchi, kuimarisha utendaji wa kifedha, na kuendelea kuwa kinara katika kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia bidhaa na huduma jumuishi za kifedha.

Mwisho .