Site icon A24TV News

PAPA MPYA HUYU HAPA ! NI MWENYE HURUMA MPOLE ANATOKA AMERIKA

Mwananchi_official Vatican. Kardinali Robert Prevost (69) kutoka Marekani amechaguliwa kuwa Papa mpya wa 267 ambapo amechagua kutumia jina kwenye wadhifa huo la Papa Leo wa XIV.

Ametangazwa kutokea katikati ya Kanisa kuu la Vatican, tangazo limetolewa na Kardinali Shemasi Dominique Mamberti.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya siku mbili za kupiga kura, akidi ya theluthi mbili muhimu kwa uchaguzi imefikiwa.
Katika siku ya pili ya mkutano mkuu wa uchaguzi wa Papa mpya leo Mei 8, 2025 imeshuhudiwa moshi mweupe kupitia dohani katika kanisa dogo la Sistine kuashiria kuwa Papa amepatikana.

Shangwe na nderemo imetanda katika Uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Petro watu wakishuhudia moshi huo ukifuka, wengi wakiwa wameshikilia simu mikononi.
Kengele zilisikika zikigongwa wakati wa tukio hilo leo kuashiria kuwa makardinali 133 wamemchagua mrithi wa Papa Francis aliyefariki dunia Aprili 21, 2025.


Moshi mweupe ulitanguliwa na mweusi uliofuka kwa nyakati tofauti mara mbili leo asubuhi na jana Mei 7, 2025 usiku. Mkutano uliofanyika kwa muda mfupi unakadiriwa kuwa saa 10 ulifanyika mwaka 1503 baada ya kifo cha Papa Pius lII. Makardinali walikutana na kumchagua Papa Julius l1. Mkutano mrefu zaidi katika historia ulichukua takribani miaka mitatu (siku 1,006) alipochaguliwa Papa Gregory X mwaka 1271.

Mwisho.