Site icon A24TV News

MWINJILISTI, EDWIN KILEO AFUNGWA MIAKA 15 JELA KWA KOSA LA KUCHOMA NYUMBA YA FAMILIA

Na Mwandishi wa A24tv.

Mahakama Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,imemuhukumu Endwin Kileo mkazi wa Kijijii cha Naibili (32)ambaye ni mwinjilist wa Kanisa  KKKT Wilayani humo,kwenda kutumikia miaka 15 jela kwa kosa la kuchoma moto nyumba yake kwa sababu ya ugomvi wa familia

Mwedesha mashitaka wa Serikali Kulwa Mungo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo Jasmin Abdul,amesema ,tukio hilo limetokea April 19 ,2025, katika Kijijii cha Naibili Wilayani humo,

Mwedesha mashitaka huyo ,amesema siku ya tukio mshitakiwa huyo alifika nyumba wanapoishi na kuingia ndani kisha kukusanya vitu mbalimbali zikiwamo nguzo na kuzichoma moto ndani ya nyumba hiyo nakutimua mbio

Kulwa amesema mwinjilisti huyo alikuwa amejenga nyumbani Kwa baba mkwe eneo la Naibili Wilayani humo,baada ya kuitilafiana na mke wake ,mke alirudi kwa wazazi wake na yeye kuondoka na nyumba ikibaki yenyewe

Baada ya jitihada za usuluishi kushindwa kuzaa matunda,ndipo jamaa aliamua kuchoma moto nyumba hiyo yenye vyumba viwili na kukilimbia kusiko julikana,lakini baada ya alikuja kukamatwa akiwa Bomang’ombe Wilayani Hai

Mwendesha mashitaka ,amesema tukio hilo ni kinyume na kifungu 319(a)sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2022

“Ni kweli tukio hilo ni kinyume na Sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 iliyafanyiwa marejeo 2022 na kesi namba 12572 /2025″amesema Kulwa

Kabla ya hukumu kutolewa Mwinjilisti alitakiwa kijitetea baada ya kukiri tukio hilo, amesema kwamba alifanya hivyo kutokana na kutoelewana na mke wake

Amesema amembembeleza mke wake huyo ili arudi nyumbani na kuendelee na maisha lakini mwanamke aliktaa kata ndipo alipochukua jukumu hilo la kuchoma moto Kwa hasira ,hivyo Mahakama imuonee huruma tayari anafamilia ya watoto wawili

Pamoja na maombi hayo hakimu huyo alimtaka kwenda kutumikia jela miaka 15 badala ya maisha baada ya kutoa utetezi wake

Wakati huo Mahakama hiyo ,imewahukumu wakazi wawili Wilayani humo kwenda jela kutumikia miaka 30 kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha

Wametaja watu hao kwamba ni Nestor Masaki (30), makazi wa koboko SanyaJuu na Athumani Muda (Noah)(30), makazi wa SanyaJuu

Hukumu hiyo imetolewa Mey 22 ,2025 na Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo,Jasmini Abdul,baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo

Mwendesha mashitaka wa Serikali Kulwa Mungo mbele ya Hakimu huyo wa Wilaya, amesema tukio hilo lilitokea mey 29 ,2024, eneo lao SanyaJuu Wilayani humo uku wakifahamu kufanya hivyo ni kosa

Kosa la unyang’anyi wa kwa kutumia silaha kinyume na kifungu 287 A cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ilifanya marejeo 2022

Awali kabla ya kutolewa hukumu mwendesha mashitaka huyo,aliomba mahakama kutolewa adhabu kali ili iwe fundishi kwa watu wanaotaka utajiri wa haraka bila kufanya kazi

Kesi hiyo namba cc,16749 ya mwaka 2024,ilikuwa na mashahidi 6 walifika mahakama hapo