Site icon A24TV News

Viongozi wa Dini Siha,watoa pongenzi kwa Taasisi Mo Dewji foundation pamoja na Godwin Mollel foundation kwa kutoa matiba bure

Na Bahati Siha,

Viongozi wa Dini Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wameipongeza taasisi ya Mo Dewji foundation kwa ushirikiano na Mbunge wa Jimbo hilo Godwin Mollel, kwa kuendesha zoezi la upimaji macho pamoja na magonjwa ya Wanawake na kupata matibabu bure.

Haya yamesemwa na Ramadhani Mollel katibu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Wilayani humo , alipofika Hospital hapo kwa ajili ya kupata vipimo.

Akizungumza na waandishi wa habari , amesema walichokifanya watu hao ni kusaidia Watanzania ni jambo jema na linapaswa kupigwa na jamii nyingine

“Ni kweli linaaswa kuigwa ,sisi tuliyopata huduma hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mungu waendelee kuwa na moyo huo na mambo yao yaweze kuendelea”amesema Mollel

Mollel amesema kuna watu wametoka nje ya wilaya na mkoa kufuata huduma hii , ndiyo uhuone huitaji ni mkubwa nadhani uku walipotoka wapo watu wenye fedha lakini hawajaona umuhimu wa kufanya zoezi kama hili,

Hivyo ni jukumu letu sisi sote kuwaombea kama nilivyosema awali kwani hatuna la kuwalipa,Mungu awatie nguvu na baraka mambo yao yaendelee na sisi tuendelee kutibiwa

Kwa upande wake Dancan Urasa Mwenyekiti wa halmshauri hiyo,pia amefurahishwa na jambo hilo la Mo Dewji kwa pamoja na Mbunge Godwin Mollel,kuamua kutoa matibabu bure, kwa waleambao walikosa huduma hii pia na kwa wale ambao hawana uwezo kupata huduma hii

Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri Haji Mnasi ,amesema kwamba leo hii wakiwa katika siku nyingine,wanatarajia kuwa na wagonjwa 6000,wa kupata huduma,akina mama pamoja na wazee, huduma hii ni muhimu,watapa na kila aliyefika anapata huduma, niwapongeze wote waliopambana kupatikana huduma hii

Mwisho.