Site icon A24TV News

Wananchi Hai watakiwa kuzingatia utaratibu wa usafi wa kinywa na meno ,kwa kupiga mswaki ili kuepuka meno kung’olewa

Na Bahati Hai,

Imebainika kuwa Watu zaidi ya 10 ung’olewa meno katika Hospital ya Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kutoka na kushindwa kutunza kinywa na meno kwa kupiga mswaki hivyo kusababisha meno hayo kuharibika

Ili kuzuia tatizo hilo unaweza kwa kufuata taratibu za usafi wa kinywa kupiga mswaki kila baada ya unapokula kituo chochote.

 

Haya yamesemwa na Daktar Emanuel Minja Mganga mfawidhi wa Hospital hiyo katika ujio wa Madaktar bingwa wa Samia ,ambao wanafanya zoezi la kupima magonjwa mbali ikiwamo maganjwa ya Wanawake hospital hapo

Akizungumza na waandishi wa habari Hospital hapo ,amewataka Wananchi kuzingatia usafi wa kinywa na meno kwa kupiga mswaki kila mara baada ya kula

“Ni kweli wanatakiwa kuzingatia usafi ,kila siku wateja zaidi ya 10 kwa upande tuu wa kung’oa wanafika,lakini Kuna upande wa kuziba tunapata wateja wakutosha pamoja na kung’arisha , tatizo ni kubwa “amesema Minja

Minja amefafanua kwa kusema kwamba ukubwa wa tatizo ili unaweza kuzuilika tuu kwa kufuata taratibu za usafi wa kinywa na meno, kwa kupiga mswaki kila mara baada ya kula kituo chochote na kupiga mswaki kabla ya kulala

Sasa hii elimu ya kupiga mswaki kila baada ya mtu unapokula wengi watu hawana ,wanafahamu Ile tuu kupiga asubuhi, lakini utaratibu haupo hivyo inabidi upige mswaki baada ya kula kituo chochote hasa vitu vya sukar

Mbali na kupiga mswaki pia ameshauti kuwaona Wataalamu wa kinywa na meno kwamba ndani ya miezi 6 ni vizuri kumuona mtaalamu ukishindwa basi ndani ya mwaka 1 njoo muone apitie kinywe chako akushauri

Amesema kwamba inawezakana wakati anapitia akagundua kuna jino limeanza kuleta shinda akaliudumia likapona ,na kubaki na meno yako

Wito wangu kwa watu wa Hai na Watu wengine kwa ujumla wazingatie usafi wa kinywaji na meno ili kuzuia matatizo hayo , usisubiri jino likuume unakose usingizi ndiyo umuone mtaalamu, wengine wanakuja mapema linazibwa na wanaochelewa linang’olewa hapana

Aidha ametoe shukrani kwa Madakitar bingwa wa Mama Samia,ni mpango ambo unasaidia sana,wengi ambao hawana uwezo kusafiri kwenda katika Hospital za Mkoa na rufaa wanafika hapa na wanaweza kupata hizo huduma hizo mwitikio ni mkubwa

Huduma ni ya kibigwa unapokelewa unafanyiwa unafanyiwa uchunguzi na kupata matibabu, wa magonjwa mbali mbali ikiwamo magonjwa ya Wanawake, watoto,mifupa,meno ,masiki pua na koo,zoezi hili limeanza Mei 12 na litamalizika Mei 17 2025

Watu wajitokeze wiki ya maana waweze kufika hapa na kuweza kupata huduma,Rais Samia Suluhuu Hassani ameshafanya kazi kubwa ya kuandaa na kuwalete ,sisi kazi yetu ni kuwatumia

Daktar Grace Matashi Dakitar bingwa wa magonjwa ya kinywaji na meno kutoka kwa Samia ,amesema kwenye huduma ya meno katika hospital hiyo kwa, Mei 12 waliihudumia wagonjwa 20 na Mei 13 wamehudumia wagonjwa zaidi ya 20 waliotoboka meno kwa wingi.

Amesema wamehudumia wote,lakini wengi wao ni vijana kuanzia miaka 20 hadi 40 ,ndiyo wapo wengi ingwa wapo Watu wazima yaliyotiboka kwenye mizizi

Kwenye hali tunayoiona hapa ,kuna haja ya elimu, wagonjwa wengi hawajui muda gani wa kupiga mswaki,mara ngapi upige,ipo haja ya Wananchi kupewa elimu afya ya meno jinsi ya kuyatunza

Mwisho