Na Bahati, Siha,
Wananchi wapatao 6740 kutoka Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro na maeneo ya jirani wamepata matibabu mbali mbali ikiwamo ya macho pamoja na magonjwa ya mfumo wa uzazi ya kina mama kutoka Taasisi ya Mo Dewji foundation
Hayo yamesemwa Me 7 ,2025 na Paschal Mbotta Mganga mkuu wa Hospital ya Wilaya hiyo ambapo, zoezi hilo limefanyika katika Hospital ya wilaya hiyo kuanzia Mei 3 hadi na kukamilika Mei 5 ,2025
Akizungumza na waandishi wa habari ,, ameishukuru taasisi hiyo kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo ili Godwin Mollel kufanikisha zoezi hilo,
“Ni kweli tunawashukuru wote waliofanikisha zoezi kufanikiwa na watu kupata huduma hii bila gharama yeyote,Mo Dewji foundation, Mbunge wetu pamoja na Serikali kwa ujumla”amesema Paschal
Paschal amesema watu hao 6740 walifika na kupata huduma,kati yao wapo waliopata miwani ya kusomea baada ya kupimwa,wapo walipata dawa za kutibu matatizo ya machona na wapo ,walifanyiwa upasuaji mdogo wa macho
Amesema huduma hiyo iliambatana na huduma ya ,magonjwa ya mfumo wa kizazi ya kina mama na kumuona Dakitar ambapo walifanyiwa vipimo na kupatiwa dawa
Amefafanua kwa kusema kwamba kati ya hao waliofanyiwa uchanguzi, lakini 15 wamekutwa na matatizo ya saratani ya shingo ya kizazi na kupatiwa tiba
Mbali na hilo pia katika zoezi hilo waliibuliwa watoto wawili wenye ugonjwa sikoseli pamoja na ugonjwa wa kichwa kikubwa , ambapo pia watasafirishwa kwenda kupata matibabu
Richard Samsoni ,ameshukuru taasisi ya Mo Dewji foundation pamoja na Serikali kutokana na huduma ya matibabu bure yaliyoitoa kwa wakazi wa Wilaya hii na nje ya wilaya ni jambo zuri,kwani kuna watu hawakuwa na uwezo wa kumudu gharama za hospital.
Aidha kwa upande wake Anna Mbise mkazi wa Wilaya hiyo,amesema kwamba alifika hospital kwa ajili ya vipimo baada ya kusikia tangazo ,lakini alipofika akaambiwa muda umemalizika na kuamua kuchukua jukumu la kurudi nyumba ,ambapo ameomba zoezi hilo lirudiwe kwani wagonjwa bado wapo
Mwisho