Site icon A24TV News

BARAZA LA MADIWANI ARUSHA LAVUNJWA RASMI ! MADIWANI WAASWA KUENDELEZA AMANI KWA WANACHI MSHIKAMANO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.

 

Na Geofrey Stephen .

Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amevunja rasmi mabaraza ya Madiwani hapa nchini na kuwashukuru madiwani kwa kufanya kazi iliyotukuka na kusema kuwa kazi yao imeandikwa kwenye kitabu cha dhahabu.

Aidha waziri Mchengerwa ameamuru madiwani kote nchini waliopatiwa vitendea kazi vya serikali ikiwemo vishkwambi kubaki navyo na hawatapaswa kuvikabidhi kwenye halmashauri Zao.

GS “Maelekezo yangu kwa katibu mkuu wa TAMISEMI vifaa hivyo walivyokuwa wakivitumiabmadiwani kama vitendea kazi wabaki navyo kwa sababu humo ndani wameweka mambo yao na sio sehemu ya mali za halmashauri”

Mchengerwa ametoa kauli hiyonleo juni 20,2025 wakati akiongea kwa njia ya simu na baraza la madiwani wa jiji la Arusha kupitia mkuu wa mkoa  wa Arusha Paulo Makonda baada ya kumuunganisha na kusema kuwa kauli hiyo ameisema kwa niaba ya mabaraza yote nchini ambayo yanakoma leo juni 20,2025.

S6 “Nakushukuru sana mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kuniunganisha na baraza la madiwani la Arusha na kufanya iwe kituo cha kutoa tamko kwa mabaraza yote nchini” 39.

Waziri Mchengerwa aliwashukuru Mameya pamoja na wenyeviti wote wa halmashauri nchini na kusema kuwa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita yametekelezwa vyema chini ya mamlaka za tawala za Mikoa na serikali za Mitaa kupitia mabaraza hayo ya madiwani.

 

Mkuu wa mkoa wa Arusha Paulo Makonda amewaasa  madiwani kwenda kusimamia amani kwenye kata zao na wasikubali kuona vurugu ya aina yoyote inatokea na na wasiwe chanzo cha virugu kwa watakao shindwa kurudi kwenye mafasi zao za udiwani katika uchaguzi ujao.

Pia Makonda alisiaitiza kwa Mkurugenzi wa jiji la Arusha ,John Kayombo pamoja na wakurugenzi wengine katika mkoa wa Arusha kuhakikisha wanawalipwa shtahiki zao kwa wakati ili watumie fedha hizo kwa majukumu yao ya kisiasa na mengineyo.

Aliwaomba kwenda kuyatangaza mema yote yaliyofanywa na serikali chininya rais Dkt Samia Suluhu hasani ambaye amekuwa mwanamageuzi wa kiuchumi nchini.

Makonda pia aliagiza wenyeviti wote wa serikali za mitaa na kitongoji kuhakikisha wanapata malipo yao kwa wakati kupitia akaunti zao na sio kutoa fedha kwa mtendaji wa kata ili awalipe na pia washirikishwe kikamilifu katika miradi ya maendeleo ya halmashauri.

Mwisho .