Na Bahati Siha,
Kaimu sheikh Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Hussein Ramadan,amewataka Viongozi wa Msikiti na kata, Wilayani humo kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi itakayo wasaidia , badala ya kusubiri misaada
Akizungumza katika eneo la Msikiti wa Sanya juu mara baada ya kupata nafasi hiyo , amesema ni kuwe na juhudi za kuanzishwa miradi ya vitega uchumi kwa namna yeyote ile ili uislamu uweze kusonga mbele.
Amesema huu sio wakati kutegemea misaada badala yake , Viongozi wanawajibu wa kutafuta njia ya kuandaa miradi ya maendeleao ambayo itakuwa na suluhisho la kupatikana kwa maendeleao ya haraka kwa Waislamu
Kwa hiyo ushauri wangu ndiyo huo,tujitahidi kuutekeleza ili kufikia malengo tuliyokusudia kwa mjibu wa katiba ya kuleta maendeleao
Aidha sambamba na hilo amewataka Viongozi hao kufahamu takwimu ya Waislamu katika maeneo yenu,hii itatupa taswara kwamba wapo wangapi ,wana watu wa aina gani kwa idadi gani
Kila kata ifahamu kuna madrasa ngapi pia kfahamu kwamba kuna shule za msingi na Sekondari ngapi, hiii itasaidia kufanya mambo vizuri
Hussein amesema jambo jingine la tatu ambalo pia ni muhimu wanapaswa kufanya ni swala la elimu, kama ambavyo Uisilamu unahimiza kusima,
Amesema Viongozi hao wanatakiwa kusimamia elimu zote mbili ,elimu ya mazingira na elimu ya muongozo kwa miguu miwili katika maeneo yao ili kupata wasomi watakao kuja kuongoza baadae
Ambapo pia amesema kutakuwa na kamati ya ukusanyaji wa zaka na sadaka, aidha amekaimu nafasi hiyo , baada ya aliyekuwa sheikh wa Wilaya hiyo Abubakar Hashimu kuachia nafasi hiyo kutokana na mambo mbali mbali.
Awali sheikh wa mkoa huo ,Shaabani Mlewa katika mazungumzo ,amewataka Waislamu Wilayani humo, kudumisha mshikamano na upendo na kuachana na migogoro isiyo ya lazima ,kwani inarudisha juhudi za maendeleao nyumba siku zote
Amesema sehemu ambapo watu hawaelewani sehemu hiyo kupiga hatua za maendeleao ni hakuna, hivyo kuwasii kuwa wamoja kuwa na ushirikiano ili kuleta maendeleao kwa waislamu Siha na Taifa kwa ujumla
Mwisho