Na Mwandishi wa A23rv
Hayo yamesemwa June 7 ,2025 Sikukuu ya Eid El-Adhhaa, na Sheikh wa mkoa huo Shaabani Mlewa iliyofanyika kimkoa katika msikiti wa Shafii Bomang’ombe Wilayani , ambapo mamia ya waumini wamehudhuria.
Akizungumza mara baada ya swala hiyo, amewataka waumini wa Dini hiyo pamoja na Wananchi kudumisha amani, upendo na utulivu kwani ndiyo msingi muhimu wa maendeleao
“Ni kweli penye upendo kuna amani kuna mshikamano,hivyo Wananchi kwa ujumla,tunahitaji kuendelea kupenda bila kujali Dini wala kabila , hasa kipindi hiki kuelekea uchanguzi mkuu “amesema Mlewa.
Mlewa amesema katika kuendelea kudumisha amani ndiyo maana Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber ametoa wito kufanya Dua Kila msikiti “amesema Mlewa
Amesema amani ikija kuharibika ,hakuna aliyejenga leo anaweza kuishi kwenye nyumba yake,hakuna aliyenunua gari yake jana anaweza kulifaidi atakimbia na kuliacha ,sisi waislmu na wasiokuwa waislmu,tunataka amani sisi
Amesema machafuko yanayotokea Nchi nyingine,yanawaza kutokea hata kwetu,hivyo Wananchi Viongozi wanawajibu wa kuendelea kutunza kudumisha matendo ya upendo,umoja kwani hiyo ndiyo moja ya silaha ya utulivu
Hivyo naomba tusiwasikilize watu ambao wanataka kutufarakanisha kwa njia yeyote ile,tuwa makini na kauli zao ,zinajenga au zinabomoa
Awali Immamu wa Msikiti huo Othumani Hamisi , ameataka waumini kuendeleza moyo wa msamaha, upendo na kusaidiana katika changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku.
Amesema kuwa Sikukuu ya Idd ni fursa muhimu ya kujenga mahusiano mema baina ya watu na kuimarisha mshikamano wa kijamii.
“Katika siku hii takatifu, tujitahidi kuwasamehe waliotukosea na kuwasaidia wenzetu wenye uhitaji. Hivyo ndivyo tunavyoweza kuishi kwa amani na upendo
Pia siku ya Leo ni kufanya mambo mazuri,sio kwenda kufanya mambo ambayo yanamchukiza Mungu hapana,ikiwamo ulevi na uzinzi
Aidha amewataka Wananchi katika uchanguzi ujao kuchangua Viongozi wenye upeo wa maendeleao,wacha Mungu,wenye uzalendo ,wasiopayuka hovyo maneno yao, kabla ya kuongea lazima upime.
Mwisho