Na Geofrey Stephen Arusha .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Kenani Laban Kihongosi Kenani Kihongosi Mtumishiwawote ametoa siku tatu kwa madereva wa vyombo vya usafiri maarufu kama bodaboda kuondoa mafataki waliyofunga kwenye pikipiki zao, mafataki ambayo yana kelele za kushtua, kelele ambazo zimekuwa ni kero kwa wananchi pamoja na watumiaji wa usafiri huo.
Mhe.Kihongosi ametoa rai, mara baada ya kujadiliana na madereva hao, kuhusu kero hiyo inavyolalamikiwa na wakazi na watumiaji wa vyombo hivyo vya usafiri kwenye maeneo yote ya mkoa huo, wakati wa kikao cha madereva wa Bodaboda, Bajaji na Magutwakwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Mkoani Arusha leo Julai 22,2025.
Hata hivyo amewataka madereva hao, kuheshimu na kuithamini kazi hiyo, kwa kuwa ni kazi kama kazi nyingine inayowaingizia kipato na kuendesha maisha yao na familia zao, hivyo amewasihi kuhakikisha wanaendesha vyombo hivyo vya moto kwa kuzingatia sheria na taratibu pamoja na kutumia fedha hizo kwa ajili ya maendeleo.
“Tumieni kazi yenu kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, tumieni fedha vizuri kwa kuwa na malengo ya kimaendeleo, nyinyi ni vijana twendeni, twendeni tukafanye maendeleo.hakikisheni
Aidha, amewataka kuwa chanzo cha usalama wa mkoa wa Arusha kwa kuwa wao wapakia watu wa aina tofauti, na kuwataka kutoa taarifa za uhalifu kwa vyombo husika, kwa kuweka uzalendo mbele badala ya kudanganywa na kujihusisha na uhalifu na sio kuwa sehzmu ya uhalifu
“Wanaofanya biashara haramu ya tatu mzuka waache mara moja, heshimuni kazi yenu ili wengine waiheshimu, Serikali inaithamini kazi yenu ya usafirishaji, wanaokwenda kinyume hawatakuwa salama” Amesisitiza.
Mwisho .