Na Mwandishi wa A24Tv Arusha .
Kesi ya madai ya sh,milioni 123 inayoikabili kampuni ya Mabasi ya Kilimanjaro Track co.ltd dhidi ya Msanii wa kizaźi kipya,Nuni Suleiman(35) Mkazi wa Dar es salaam, imeunguruma katika mahakama ya wilaya Arusha.
Shahidi wa kwanza katika shauri hilo la Madai namba 36 la mwaka 2022,
Nuni Suleimani,mbele ya Hakimu Mwandamizi Wilaya ya Arusha,Bitony Mwakisu ,amedai mahakamani hapo kuwa kampuni hiyo ya Kilimanjaro imejinufaisha kwa kutumia nyimbo yake ya Tabasamu Tanzania kujitangaza kibiashara kupitia mitandao ya kijamii bila idhini yake na kudai fidia ya kiasi hicho cha fedha.
Alidai hayo wakati akiongozwa na wakili wake,Lillian Justo ,akidai alianza kazi ya Usanii wa nyimbo mwaka 2015 na nyimbo hiyo ya Tabasamu Tanzania, aliikamilisha kuitunga na kuiachia kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari mwaka 2021 na baadaye alikabidhiwa cheti cha umiliki wa nyimbo kupitia Chama Cha Hakimiliki (COSOTA).
“Nipo Mahakamani hapa kuiomba mahakama kuiamuru kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Track co.ltd kunilipa fidia ya sh, milioni 123 baada ya kutumia wimbo wangu kwenye matangazo yake ya Biashara bila kunishirikisha “
Alidai kwamba alitambua kampuni hiyo kutumia wimbo wake baada ya kuona kupitia akaunti yao ya Instagram wakitangaza huduma zao mbalimbali ikiwemo usafirishaji ,huduma za maradhi na mgahawa wa chakula .
Wakili Lilian alimwomba mteja wake kuvitambua baadhi ya vielelezo ikiwemo Flash iliyokuwa na nyimbo hiyo,pamoja na cheti cha COSOTA na kuviwakilisha mahakamani ili vitumike kama vielelezo.
Mahakama ilipokea vielelezo hivyo baada ya wakili wa mjibu maombi Godluck Michael kudai hana pingamizi na baadaye nyimbo hiyo iliyokuwa kwenye flash ilichezwa mahakamani hapo kupitia runinga kubwa iliyokuwepo ndani ya mahakamani.
“Niliona nyimbo yangu inatumiwa kutangaza biashara zinazotolewa na kampuni hiyo ya Kilimanjaro ,niliirekodi kupitia simu yangu ya mkononi na baadaye nilipeleka malalamiko yangu COSOTA”
Anaeleza kwamba COSOTA iliandika barua ya wito kwa kampuni ya Kilimanjaro lakini baada ya kukutana katika ofisi hizo za COSOTA huku kampuni hiyo ikiwakilishwa na Kondakta wake ,hawakufikia mwafaka.
“Niliamua kuiandikia barua kampuni hiyo( Demand Note) ya kusudio la kuishitaki nikitaka inilipe sh, milioni 123 ndani ya siku 14,hata hivyo hawakujibu chochote na baada ya muda huo niliamua kuja hapa mahakamani kudai haki yangu”
Akihojiwa na wakili,Lilian kuhusu uhalali wa akaunti hiyo na kampuni ya Kilimanjaro track co.ltd ,alisema alijiridhisha kuwa akaunti hiyo inamilikiwa na Kampuni hiyo kutokana na kwamba mawasiliano ya simu zote katika vituo vyote vya mabasi hayo nchini yalikuwa yameweka humo.
Nuni pia alidai mahakamani hapo kuwa siku moja baada ya kampuni hiyo kupelekewa barua ya wito COSOTA tangazo hilo liliondolewa mtandaoni na pia uongozi wa kampuni hiyo haujawahi kujitokeza hadharani kukanusha kuwa akaunti hiyo sio mali yao na anwani zote zipo na vituo vya Mabasi viliolodheshwa katika akaunti hiyo.
Akihojiwa maswali ya dodoso na wakili anayeiwakilisha kampuni ya Kilimanjaro Track co.ltd , Goodluck Michael kama kweli ameiona nyimbo yake hapa mahakama ama ameona tangazo
Nuni alidai ameisikia ikiwa kwenye tangazo la biashara la kampuni ya Kilimanjaro.
Hakimu Mwakisu aliahirisha kesi hiyo hadi septemba 9 mwaka huu ambapo upande wa mashtaka utaendelea na shahidi mwingine siku hiyo.
Mwisho .