Siha
,Mganga Mkuu wa hospital ya wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Paschal mbotta,ametoa shukurani kwa Jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania (JMAT), Wilayani humo kwa kuona umuhimu wa kukusanya damu vijiji kwa ajili ya wagonjwa wanaofika hospital hapo wakiwamo kina mama wajawazito
Haya yemesemwa katika hitimisho ya maridhiano day katika hospital ya Wilaya hiyo, ambapo shughuli mbali mbali zimefanyika ikiwamo kupanda miti, utoaji wa damu na kuwatembea wagonjwa sambamba na kufanya maombi ibada ya kuwaombea wagonjwa
Akizungumza na Viongozi Jumuiya hiyo ngazi ya kata , Wilaya na mkoani katika ukumbi wa hospital hiyo , amesema kitendo walichokifanya ni cha kuokoa maisha ya watanzania ni jambo jema na linapwa kuigwa.
Paschal mesema kitendo cha kuacha shughuli zao na kwenda uko kijijii kutuletea hapa hospital ya wilaya damu kusaidia kuokoa maisha ya watanzania, wajawazito wenye upungufu wa damu, wagonjwa waliopata ajali ni jambo la kiungwana sana
“Jana wamekusanya na kutuletea chupa 18 za damu hivyo unaweza kuona ni namna gani unaweza kwenda kuokoa kubwa ya wagonjwa vituo vyetu vya Afya”amesema Paschal
Mwaka jana walifanya maadhimisho haya pia walichangia damu na kufanya shughuli mbali mbali ikiwamo kupanda miti na kufanya usafi pamoja na kutembea wagonjwa
Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka, amesema mbali na kuchangia damu, Jumuiya hiyo imekuwa ikitatua changamoto mbali mbali migogoro ikiwamo ya Aridhi ,ndoa na mirathi.
“Ni kweli kazi ambayo mnafanya kuhakikisha jamii yetu inakuwa salama yenye amani maelewano icho ndicho kinachotakiwa ,kwa hiyo kupitia kwenu naomba tuendelee kuongeza.. jitihada za kuwafanya watu waishi vizuri, tuendelee kushirikiana”amesema Timbuka
Awali Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoani hapa Jones Mola , amesema jukumu la Jumuhiya hiyo,inafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali,wanasiasa , Viongozi wa Dini kutatua migogoro na kukuza jamii yenye amani
Ambapo amesema maridhiano day mwaka huu yatafanyika mkoani Arusha,ni mgeni rasmi anegemewa kuwa Rais Samia Suluhuu Hassani
Mwisho