Dar es Salaam.
Na Mwandishi wa A24Tv.
Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupa maombi ya Halima Mdee na wenzake kutokana na kasoro katika jina la mjibu maombi wa kwanza.
Halima ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na wenzake waliomba kibali cha kupinga kufukuzwa uanachama wa Chadema katika mahakama hiyo.
Wajibu maombi walikuwa Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Chadema kupitia jopo la mawakili wake linaloongozwa na Peter Kibatala waliweka pingamizi wakiiomba Mahakama hiyo isiyasikilize maombi hayo, wakidai kuwa yana kasoro za kisheria huku wakibainisha hoja sita.