Author: Geofrey Stephen

Na  Mwandishi wa A24tv . Imeelezwa kwamba Tanzania ina aina mbalimbali za madini ya viwandani ambapo kwa mujibu wa toleo jipya la pili la kitabu cha madini viwandani kilichoandikwa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kimeonesha aina 43 za madini viwandani ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya viwanda na ufungamanishaji wa sekta za kiuchumi nchini. Hayo yamebainishwa leo Novemba 20,2024 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati wa uzinduzi wa kitabu cha madini ya viwandani toleo la pili , ikiwa ni siku ya pili Mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji Sekta ya Madini 2024. Waziri Mavunde…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv Siha, Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Ronald Ulomi mkazi wa kijijii Ormelili (34),kwa tuhuma za kumuua bibi yake mzaa mama Akanashe Mushi(85),kwa kupiga kichwani kwa kutumia na nyundo na jiwe na kumsababishia kifo chake Akizungumza tukio hilo November 18 ,2024,Kamanda wa Polisi mkoa hapa Simon Maigwa, amesema tukio hilo limetokea November 16 ,2024, katika eneo la Ormelili Wilayani Siha mkoani hapa Tumesha mkamata ,alikuwa anapelekwa hospital na mama yake mzazi, Rahel Munisi ,sasa wakati wanampeleka akawatoroka na kurudi nyumbani,mke wake akamfungua kamba , Ambapo alichukua nyundo na kumpiga bibi kuchwani na kuondoka chini ,baada ya…

Read More

Na Bahati Siha, Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Christopher Timbuka, amesema wanafunzi kadhaa wa kidato cha sita shule ya Sekondari Sanya Day,wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa kuleta vurugu shuleni hapo ikiwa ni pamoja na kutaka kuchoma nyumba ya mwalimu Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu,amesema tukio hilo limetokea November 17 ,2024,nakuwataka wanafunzi kuzingatia yaliyowaleta shuleni “Ni kweli tukio limetokea la wanafunzi kutaka kuchoma nyumba ya mwalimu jambo ambalo ni la kuuzunisha na sasa wapo chini ya vyombo vya Sheria”amesema Timbuka Timbuka anasema ,kuna wanafunzi alikutwa na simu siku hiyo hapo shuleni na walinzi walimuona…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . WATAALAMU wa ununuzi na Ugavi hapa nchini wametakiwa kuwa wazalendo na kuzingatia maadili,weledi,kanuni na taratibu katika kutekeleza majukumu yao . Hayo yamesemwa leo mkoani Arusha na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Missaile Musa wakati akifungua mafunzo kwa wataalamu wa manunuzi yanayoendelea mjini hapa. Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi(PSPTB)na kushirikisha wataalamu wa sekta hiyo toka halmashauri zote na sekretarieti ya mkoa wa Arusha. Musa amewataka kujiepusha na vitendo vya rushwa na kujikita zaidi katika kusimamia kikamilifu fedha zote za umma zinazotengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali. “hakikisheni…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv Arusha. Benki ya NMB imefanikiwa kuwapa semina watumishi wa umma wanaokaribia kustaafu juu ya fursa za kiuwekezaji wanazoweza kujiongezea kipato kutokana na fedha za mafao wanayotarajia kupokea. Akizungumza na watumishi wa umma zaidi ya 150 wanaokaribia kustaafu Mkoani Arusha, Meneja Mahusiano amana za wateja kutoka Benki ya NMB Monica Job amesema kuwa wameamua kutoa Elimu hiyo ili kuwaepusha wastaafu na matapeli. “Leo tumekuja kuwajulisha wastaafu watarajiwa juu ya masuluhisho ya kifedha tuliyonayo kwa ajili yao kuanzia miamala ya kawaida, akaunti maalumu ya wastaafu tunayoiita ‘Wisdom akaunti’ lakini pia mikopo mbalimbali” amesema Monica. Monica amesema, katika kuhakikisha…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Novemba 18, 2024 jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano katika masuala ya elimu, hususan elimu ya amali ufundi. Waziri Mkenda ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara inaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mageuzi ya elimu, ikiwa ni pamoja na kuweka nguvu kuimarisha elimu ya amali ufundi inayolenga kuwezesha ujuzi kwa vijana Amesema China na Tanzania zina historia chanya ya ushirikiano katika sekta ya elimu, na kwamba Serikali ina shauku kubwa kushirikiana…

Read More

1.0 Utangulizi Taarifa hii fupi kwa umma inakuja baada ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kufanya ziara mwezi Novemba 2024 katika Tarafa ya Ngorongoro, Wilayani Ngorongoro. Lengo kuu la ziara ilikuwa ni kuangalia hatua zilizochukuwa na Serikali katika kutatua changamoto zilizoainishwa katika ripoti ya watetezi wa haki za binadamu ya mwaka 2023 iliyoonyesha kuzorota kwa huduma za kijamii katika Tarafa ya Ngorongoro Wilayani Ngorongoro mkoani Arusha pamoja na agizo la Mhe Rais Samia Suluhu Hassan la kurejeshwa kwa huduma aliyoitoa mwezi September 2024 baada ya maadamano ya wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro. Katika ziara hii,…

Read More