Na Geofrey Stephen – Tanga.
Waziri wa Viwanda na Biashara Suleman Jafo amewataka viongozi kutatua changamoto za wananchi kibiashara ili kuweza kukuza uchumi wa taifa maana tayari miundombinu wezeshi ya kibiashara imeshawekwa na Mh Rais Samia Suluhu Hassan na sasa ni wakati wa Watanzania kunufaika na biashara zao.
Amesema hayo leo Agosti 22, 2024 wakati akizungumza na watumishi wa Jiji la Tanga mara baada ya kutembelea viwanda mbalimbali Jijini Tanga na kufungua kituo cha Uwezeshaji wananchi Mkoa wa Tanga.
Waziri Jafo amewataka viongozi kutunza kituo hicho ili kiweze kuleta mafanikio kwa watanzania kama ilivyo kusudiwa na kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto za wafanya biashara Mkoani humo.
“Niwaombe sana viongozi wenzangu tuweze kutatua changamoto za wananchi Mhe, Rais ametuamini sana na sisi tunapaswa kumlipa uaminifu kwa utendaji kazi bora kwa wananchi wetu”. Amesema Jafo.
“Katika kitu hiki cha uwezeshwaji nilicho kifungua leo ninaomba kikawe ni majibu tosha kwa watanzania na wafanya biashara wa Mkoa huu na kiweze kuleta tija. Tayari Rais Samia ameshaweka miundo mbinu sahihi ya Kibiashara na bandari hii inakwenda kufunguliwa kuwa njia sahii ya usafirishaji waya za kopa hii itachochea ukuaji uchumi katika Mkoa huu”. Ameongeza Waziri Jafo.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanga Japhari Kubecha, ameeleza kuwa kwasasa uwekezaji umefanywa na serikali ni mkubwa hasa katika upanuzi wa bandani pamoja na rwli ya SGR unakwenda kuwa kiunganishi kikubwa kwa afanya biashara hapa nchini hasa wa Mkoa wa Tanga.
Aidha Kubecha amewataka wafanyabiashara kutunza miundombinu iliyowekwa ili kuweza kutumika kwa vizazi vya sasa na vijavyo katika ujenzi wa taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Eng. Juma Hamsini amesema kwasasa anakwenda kilifungua Jiji la Tanga kibiashara ili kuweza kukua kiuchumi kutokana na uwekezaji uliyo fanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuigungua bandari ya Tanga kibiashara.
Eng. Hamsini ameeleza kuwa moja ya mikakati yake ni kulifanya Jiji la Tanga kuwa mlango wa kibiashara katika ukanda wa kaskazini na kuahidi kukitunza kituo cha Kibiashara hicho kilicho funguliwa kwa kuongeza madawati mbalimbali ya ushauri na uwezeshwaji kwa wananchi.
Mwisho