Site icon A24TV News

TUME YA MADINI YAIBUKA MSHINDI WA TATU KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

Na Mwandishi wa A24Tv Geita

Tume ya Madini leo Oktoba 08, 2022 imeibuka mshindi wa tatu kwenye Kundi la Taasisi Wezeshi za Serikali katika Sekta ya Madini kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Bombambili mjini Geita.

Kikombe cha ushindi kimekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ufungaji wa maonesho hayo.

Ili kuendelea kutoa huduma zaidi kwa wananchi wa mkoa wa Geita na mikoa ya jirani, zimeongezwa siku mbili za maonesho hayo.