ATC na RUWASA zasaini Mkata.
Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) wakishirikiana na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wamesaini Mkataba wa makubaliano wa utengenezaji wa Dira za Maji za Malipo ya kabla ya matumizi (pre-paid). Mkataba ambao ulishuhudiwa na Waziri wa Maji Mhe. Juma Waweso na Naibu Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Juma Kipanga.Akizungumza wakati wa kusaini Mkataba huo,
Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso amesema kuwa, uwepo wa Wizara ya Elimu, sayansi na Teknolojia kupitia ATC umekuwa Msaada mkubwa kwa Taasisi zetu hapa nchini.“Leo hii tungewaza kuagiza Dira za maji kutoka nje ya Nchi lakini tukasema ni vema kukatumia wataalamu wetu wa ndani wenye ujuzi katika kusaidi taifa letu” alisema,
Mhe. Awezo na Ameongeza kuwa, Dira zitakazo tengenezwa ziwe bora na baadae soko litakapokuwa kubwa gharama zake ziwe nafuu ili tuweze kutatua changamoto ya huduma za maji vijijini.Kwa upande wake, Naibu Waziri elimu, sayansi na teknolojia Omary Kipanga amesema uwepo wa Wizara katika hafla ya kutiaji Saini ni kwa sababu uwepo ya ATC ambayo ni taasisi iliyopo chini ya wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.“niliwahi kutembelea taasisi yetu ya ATC pale Arusha na kujionea kwa jinsi gani teknolojia hii ya malipo ya kabla inavyofanya kazi” alisema Naibu Waziri Kipanga.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Mhandisi Clement Kivegalo amesema mkataba huo, ATC katika hatua za awali itatakiwa kubuni na kufunga Dira za maji zipatazo 100 ambazo zitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya majaribio kwa kipindi cha miezi sita
“kuna faida za kutumia wataalamu wetu wa ndani katika kubuni na kufunga Dira za maji. Hii itaboresha ushirikiano wa taasisi zetu za umma na binafsi katika utoaji wa huduma za maji vijijini” alisema mhandisi KivegaloChuo cha Ufundi Arusha kinatarajiwa kuanza rasmi utengenezaji na ufungaji wa dira za maji za malipo ya kabla ya matumizi zipatazo 100 ambazo zitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya majaribio(Pilot Study) kwa kipindi cha miezi. Dira hizi zimebuniwa na wataalam kutoka chou cha Ufundi Arusha.