Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv . Polisi kata NGARENARO jijini Arusha Mkaguzi Msaidizi wa polisi TADEY TARIMO ametoa rai hiyo kwa wanafunzi wa shule za msingi na secondary katika kata hiyo wakati akitoa Elimu juu miradi mbalimbali ya polisi jamii. A/INSP TARIMO amewataka wanafunzi kutokua na hofu waonapo viashiria vya vitendo vya ukatili dhidi yao au kwa watu wao wa karibu na badala yake watoe TAARIFA mapema ili hatua ziweze kuchukuliwa. Sambamba na hilo Mkaguzi huyo amewahakikishia Usalama wanafunzi hao pindi watoapo TAARIFA za Ukatili na uhalifu mwingine unaotokea na kutendeka katika maeneo yao. Mwisho A/INSP TARIMO amewataka wanafunzi kuepukana na…

Read More

Siha, Baraza kuu la Waislamu Tanzania ( BAKWATA), Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro limesema litampokea mtu yeyote yule anayekuja na jema ambalo lipo ndani ya Aya na hadidhi na kushirikiana naye bega kwa bega katika kuwaletea maendeleao ya Waislamu na jamii kwa ujumla. Haya yamesemwa March 25 2025,na Sheikh wa Wilaya hiyo, Abubakar Hashimu wakati wa zoezi la ufuturishaji kiwilaya lililofanyika katika Msikiti wa SanyaJuu kiwilaya ambalo lilibebwa na Tumsifu Kweka mjumbe wa halmshauri kuu ya CCM mkoa na mkutano mkuu wa CCM Taifa Sheikh Akizungumza mara baada ya zoezi hilo kuitimishwa , amesema Ofisi ya Baraza hilo Wilayani humo itampokea…

Read More

Siha, Wananchi wa kijijii cha Sanya Hoyee Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wameomba Viongozi wa maeneo hayo kuzuia upigwaji Muziki katika baar ambazo hazina sehemu maalumu ya kuzuia sauti(Sound proof)ili kuepusha usumbufu kwa jamii Maombi hayo yamekuja baada ya kuwepo upigwaji wa mziki mkubwa na kusababisha kero hasa nyakati za usiku ambapo watoto, wagonjwa, pamoja na wanafunzi kushinda kupata usingizi Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, wameomba wausika kufunga vyombo hivyo maalumu vya kuzuia sauti. “Ni kweli kero kubwa wanashindwa kupata usingizi , Watoto, wagonjwa wazee na wengine,Muziki unapigwa Baar na hata baadhi ya nyumba za ibada ,ni usumbufu…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv .Same Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, imefanya operesheni maalum wilayani Same, mkoani Kilimanjaro kuanzia tarehe 19 hadi 25 Machi 2025. Katika operesheni hiyo, ekari 285.5 za mashamba ya mirungi zimeteketezwa na watuhumiwa saba (7) wamekamatwa, akiwemo kinara wa biashara haramu ya mirungi nchini aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu, Interindwa Zinywangwa Kirumbi, maarufu kwa jina la mama Dangote. Akizungumza baada ya operesheni hiyo, Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo, amesema kuwa, mama Dangote ni mzalishaji na msambazaji mkubwa wa dawa za kulevya aina ya mirungi…

Read More

Na Pamela Mollel,Arusha Mhashamu Baba Askofu Mkuu wa kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (K.K.A.M)Oscar Ulotu amemsimika rasmi Dkt.Philemon Mollel,mfanyabishara maarufu(Monaban) kuwa Baba Askofu Mteule wa Dayosisi ya Arusha. Baba Askofu Mollel amesimikwa Machi 23,2025 kwenye ibada maalum iliyofanyika katika kanisa la K.K.A.M Mto wa Mbu-Kigongoni Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali na vyama vya Siasa,waumini pamoja na kwaya mbalimbali ambazo zilitumbuiza katika hafla hiyo iliyokuwa ya kipekee. Akizungumza wakati wa kumsimika Askofu Mkuu,Oscar Ulotu ambapo alimkabidhi fimbo kama ishara ya kuongoza waumini wa kanisa hilo,alimkumbusha Askofu Mollel kuwa fimbo hiyo siyo…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. NCAA. Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya Umma (PIC) imefanya ziara katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro tarehe 23-24 Machi, 2025 na kuipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa uboreshaji wa miundombinu ya Utalii na ujenzi wa jengo la Makao makuu ya NCAA nje ya Hifadhi. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya Umma Mhe. Augustine Vuma (Mb) amesema kuwa, kamati inaipongeza NCAA kwa ujenzi wa Jengo la Makao makuu ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha shughuli za uhifadhi na kupunguza shughuli za kibinadamu katika hifadhi ya…

Read More