Juni 3/2022
ARUSHA
Na Geofrey Stephen
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk.Pindi Chana ameihakikishia Dunia sekta ya utalii nchini na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imefunguka kwa sasa,baada ya kupungua kwa janga la Uviko 19 na kuiomba kutembelea vivutio vilivyopo.
Akizungumza jana wakati akifungua maonyesho ya kimataifa ya Utalii ya Karibu- Kili Fair kwa niaba ya Waziri Chana,Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki alisema kwa sasa masharti yamepungua ya janga hilo na maeneo mengi yanafikika kiurahisi.
“Maonyesho haya watasaidia kutangaza Dunia kuwa sasa utalii umefufuka tena kwa Tanzania na nchi za EAC na natoa wito watu wote mtembelee vivutio vilivyopo,”alisema.
Alisema utalii ulipitia purukushani nyingi hivyo kwa sasa hali yake unarudi baada ya kupungua kwa janga hilo na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mstari wa mbele kutangaza vivutio hivyo kupitia Filamu ya Royal Tour.
Pia alipongeza waandaaji wa maonyesho hayo ambayo yamekutanisha wadau wa utalii wa nchi za EAC na Duniani kwa lengo la kumuunga mkono Rais Samia kutangaza vivutio vilivyopo.
Alisema endapo kila mmoja atashiriki kutangaza vivutio hivyo kila mmoja atanifaika na sekta hiyo
.Naye Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanziba,Rahim Bhaloo alisema kwa sasa Tanzania na nchi za EAC zipo tayari kupokea watalii na wameshaweka mazingira rafiki kwao ikiwemo kuimarisha usalama, kwa wageni watakaotembelea kwenye nchi hizo.
“Tanzania Bara kuna utalii wa Mbuga na Zanziba kuna utalii wa Bahari kupitia fukwe zake,lakini pia tunashukuru Rais Samia kupitia Fulamu take ya Toyal Tour tumeanza pokea wageni maarufu duniani na maonyesho haya yataongeza idadi ya wageni zaidi,”alisema.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kili Fair Dominic Shoo ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo alisema mwaka huu wamepata washiriki zaidi ya 8000 kutoka nchi mbalimbali duniani.
Aliomba watanzania kuja katika maonyesho hayo ambayo kunamengi ya kujifunza kupitia semina zinazotolewa.
Mkuu wa Mkoa Arusha John Mongella alisema mkoa huo umejipanga kupokea watalii na wanazidi kuimarisha usalama kwa wageni wanaotembelea vivutio vyao.
Aidha kwa upande wake Meneja wa Mauzo na Masoko kutoka kampuni ya uuzaji wa nyama hapa nchini kiwanda cha Happy Sousage Bi Neema Mboya, Amesema katika kuendeleza sekta ya utalii hapa nchini wao kama happy sousage wamepqnga vyema kuhakikidha bidhaa wanazo zalisha ziwe kwa wingi iki kumudu soko la utalii hapa nchini.
Pia Mboya ameeleza kuwa bidhaa zao zinatokana na mifugo halisi wanaofungwa hapa nchini na watanzania na wanatumia mifugo iliyo bora ili kukidhi masoko mbali mbali ya bidhaa hiyo ambayo ni pendwa sana kwa watanzania na wageni kutoka mataifa mbali mbali.
Akitoa ufafanuzi katika sekta ya Uwekezaji Meneja wa mauzo kutoka kowanda cha Happy Sausage jijini Arusha Bi Neema amesema Mahusiano kanda ya kaskazini kwamba ili kukuza sekta ya utalii wamejipanga kutoa Uduma mbali mbali kwa wafanya biashara wa utalii ili kuweza kukabiliana na changamoto za kibiashara ikiwa ni pamoja na ulaji wa Nyama safi na salama katika biashara hiyo ya utalii.
Bidhaa zinazo zalishwa na kiwanda cha happy Sausage cha jijini Arusha .
Mwisho