Na Geofrey Stephen_ Arusha
Wanawake kutoka Nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo nchi uanachama zinazo unda Jumuiya ya Afrika Mashariki ( EAC ), SADIC, COMESA na ECOWAS wametakiwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi hasa katika uongozi wa kisiasa katika Nchi zao ili kuweka usawa katika nyanja ya uongozi.
Hayo yameelezwa na Mhe, Anastazia Wambura, Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mtwara wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wanawake viongozi Jijini Arusha, kwa niaba ya Spika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson, Mkutano huo unaofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa bunge wa EAC, Lengo kubwa katika Mkutano huo ni kujadili changamoto zinazo mkabili mwanamke na namna bora ya kuwawezesha kukabiliana nazo.
Mhe, Anastazia ameeleza kuwa ni vyema wanawake wakapata nafasi za uongozi kwani mwanamke ndiye mzazi,mlezi, mtu mwepesi wa kubaini matatizo katika jamii pia ni chombo kikubwa Cha amani,Pia wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazozuia wao kuingia katika nyanja za uongozi wa kisiasa ikiwemo kukabiliwa na shughuli nyingi za kifamilia.
“Mambo mengine ni Mila, desturi na tamaduni ambazo zinawaona wanawake ni viumbe duni ambao hawawezi kutoa maamuzi kwahiyo mambo kama haya ndo yanaenda kujadiliwa lakini pia kubadilishana uzoefu kati ya nchi na nchi kuona wao wamewezaje kwa mfano Rwanda utaona wao wako karibia asilimia 64 ya wabunge ni wanawake lakini kwetu Tanzania ni asilimia 37 na wapo ambao wapo chini ya hapo hivyo tutabadilulishana uzoefu,” Alisema Mhe, Wambura.
“Tutaangalia kwa pamoja tufanye nini ili tuweze kuhakikisha kwamba wanawake Afrika wanapata nafasi za uongozi kwani tunataka tuwe asilimia 50 kwa 50 lakini kwasababu ya hizi changamoto ndio maana bado hatukafikia lakini pia ni nafasi za wakereketwa kuhakikisha kwamba nafasi za wanawake zinaongezeka, bado nchi nyingi hazijawaweza kuweka kwenye mitaala lakini ni mapendekezo”. Alisistiza Mhe Wambura
“Kwamba watoto wanapoingia darasa la kwanza hadi lasaba wajue kuwa mwanamke ni mtu wa muhimu katika kuiendeleza jamii kwahiyo wasiwe na mtadhamo hasi dhidi ya mwanamke, watakapowekewe kwenye mtaala moja kwa moja akiwa mkubwa akiambiwa nenda kapige kura anakuwa akijua niliambiwa kuwa mwanamke ni kiumbe muhimu katika kuleta maendeleo kwenye jamii,” Alieleza Mhe, Wambura
Kwa upande wake Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda, Dkt , Rebecca Kadaga , alieleza kwamba amekuwa Spika wa Bunge la Uganda kwa miaka kumi na ameshiriki katika mkutano huo ili kubadilishana uzoefu juu ya kipi wafanye ili wanawake waweze kupata nafasi za uongozi ikiwemo kukagua mambo mbalimbali ya serikali ikiwemo Bajeti na uwakilishi wa wanawake kwa kuhakikisha asilimia 30 wanashiriki.
“ Tunataka kuhakikisha kuwa katika maeneo yetu kunakuwa na shule sahihi kwaajili ya watoto wa kike kwahiyo tupo kushauri kuhakikisha tunapaza sauti kwa pamoja na kufikia malengo ya kidunia katika nchi zetu za kuleta usawa katika mambo mbalimbali ikiwemo nafasi za uongozi,”Alisema Dkt Kabaga.
Mmoja wa wanaharakati wanaopigania haki za wanawake kutoka Congo DRC Agnes Sadiki ambaye pia alishawahi kuwa waziri wa uchukuzi nchini humo, msemaji wa serikali na waziri wa bajeti alisema kuwa amefurahi kuona nchi nyingi zinaendea kupiga hatua katika kuwashirikisha mwanamke katika ngazi za uongozi na kutolea mfano Tanzania Zambia na Rwanda.
“Itatubidi katika nchi yetu ya Congo kuomba wakuu viongozi ambao nao wamesaini mikataba mbalimbali ikiwemo ya protocoli ya MAPUTO na nyinginezo ambazo zinaomba kumshirikisha mwanamke katika kila kitu ambacho kina lenga amani kwasababu hakuna uongozi bila amani lakini pia katika chaguzi kwani Congo tunajitahidi kuwa nchi yenye demokrasia,” Alisema Sadiki
“Tutaenda katika uchaguzi hivi karibuni kwahiyo ni sharti wakuu viongozi kama walivyosaini ile mikataba na kukubaliana kumweka mwanamke katika ngazi ya uongozi waweze kuzitekeleza lakini inabidi pia wanawake wao wenyewe wafanye juhudi za kuingia katika uongozi kwani wanastahili kuongoza pamoja na wanaume lakini pia watambue kuwa hawataweka tu kwa sababau ni wanawake bali wawe wanawake wanaostahili,” Aliongeza Sadiki.
“Wawe wanawake wenye ujuzi, wasomi, wamelimika lakini vilevile awe na jitihada ya yule ambaye anastahili kuongoza kwa niaba ya wananchi kwa faida ya akina mama na raia wengine,” Alisisitiza Sadiki.
Naye Katibu Mkuu wa umoja wa wanawake wa Bunge la Jumuiya ya Africa mshariki (EALA) Fatma Ndagiza, Alisema kuwa mkutano huo ni wa siku tatu ambapo lengo ni kuwapa nafasi wanawake waliopo katika siasa nafasi na kubadishana mawazo na uzoefu hasa jinsia gani walifika katika nafasi walizonazo zinazotoa uamuzi, kuelezana changamoto na ninamna gani wataweza kuzikabili changamoto hizo.
“Tunatarajia kuwa baada ya mazungumzo haya tutakuwa na mikakati mbalimbali ikiwemo ya kujitahidi kubadili Katiba za nchi zetu au kama wawakilishi tuweze kufuatilia na kuhoji serikali zetu ili wanawake wawe na mchango kwa maendeleo ya taifa zao lakini pia wawe na wanawake wengi katika ngazi za siasa,” Alisema Ndagiza.